Pata taarifa kuu

Mkuu wa AU aituhumu Israeli kwa mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza

Nairobi – Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat, ameituhumu Israeli kwa kile anachosema ni mauaji ya halaiki dhidi ya raia wa Palestina.

Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.
Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Faki ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuanzisha uchunguzi baada ya watu waliokuwa wanataka kupewa chakula cha msaada kushambuliwa na Israeli.

Mamlaka huko Palestina inasema watu 100-waliuawa katika shambulio hilo wengine 750 wakiripotiwa kujeruhiwa.

Wanajeshi wa Israeli waliwafyatulia risasi raia wa Palestina siku ya Alhamis waliokuwa wanataka kupata sehemu ya chakula cha msaada.

Tukio limetokea baada ya shirika la mpango wa chakula duniani WFP kuonya kuwa iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa, huenda raia wa Kaskazini mwa Gaza wakakabiliwa na baa la njaa.

Israeli imeendelea kuetekeleza mashambulio katika Ukanda wa Gaza ikisema inawasaka wapiganaji wa Hamas.
Israeli imeendelea kuetekeleza mashambulio katika Ukanda wa Gaza ikisema inawasaka wapiganaji wa Hamas. AP - Hatem Ali

Jeshi la Israeli limesema kulitokea mkanyagano baada ya maelfu ya raia wa Gaza kuzunguka msafara wa malori 38 ya misaada, tukio ambalo lilisababisha kutokea kwa vifo, baadhi ya raia pia wakijeruhiwa wengine wakikanyagwa na malori hayo.

Viongozi mbalimbali duniani, akiwemo rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamelaani kitendo cha wanajeshi wa Israeli kuwapiga risasi na kuwauwa Wapalestina zaidi ya 100 waliokuwa wamejitokeza kupokea msaada wa chakula Kaskazini mwa Gaza.

Emmanuel Macron ni miongoni mwa viongozi ambao wamelaani hatua hiyo ya Israeli.
Emmanuel Macron ni miongoni mwa viongozi ambao wamelaani hatua hiyo ya Israeli. AFP - GONZALO FUENTES

Riyad Mansour, Balozi wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa, amesema Baraza la Usalama linapaswa kupitisha azimio la kusitisha vita kwenye ukanda wa Gaza.

Jeshi la Israeli limejitetea kuwa, lilitekeleza shambulio hilo baada ya kuhisi kuwa idadi kubwa ya watu waliojitokeza kupata msaada wa chakula wakati huo ilikuwa ni hatari kwa usalama wao.

Tangu kuanza kwa vita Oktoba mwaka uliopita, mpaka sasa watu zaidi ya Elfu 30 sasa wamepoteza maisha kwenye vita vinavyoendelea kati ya jeshi la Israeli na kundi la Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.