Pata taarifa kuu

Stéphane Séjourné kuzuru Israel na Ukingo wa Magharibi siku ya Jumatatu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stéphane Séjourné amesema atazuru Israel na Ukingo wa Magharibi siku ya Jumatatu. Katika ziara yake, Stéphane Séjourné atakutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Israel Katz, Kiongozi wa Upinzani Yair Lapid, Waziri wa Masuala ya Mikakati Ron Dermer na Mshauri wa Usalama wa Taifa Tzachi Hanegbi.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imetangaza kwamba Stéphane Séjourné pia atakutana na familia za mateka na watu waliotoweka wenye uraia wa Ufaransa.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imetangaza kwamba Stéphane Séjourné pia atakutana na familia za mateka na watu waliotoweka wenye uraia wa Ufaransa. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imetangaza kwamba Stéphane Séjourné pia atakutana na familia za mateka na watu waliotoweka wenye uraia wa Ufaransa. Ziara yake itakuwa sehemu ya safari ya siku nne katika Mashariki ya Kati, ambapo pia atazuru Misri, Jordan na Lebanon.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anatarajiwa katika Mashariki ya Kati siku ya Jumapili kuunga mkono mazungumzo juu ya mapatano mapya kati ya Israel na Hamas. Atafanya ziara yake hadi Qatar, Misri, Israel, Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na nchini Saudi Arabia.

Kusitishwa kwa misaada ya kibinadamu huko Gaza na kubadilishana kwa mateka na wafungwa wa Kipalestina kutazingatiwa. Siku ya Jumamosi afisa mkuu wa Hamas alisema kuwa Israel inachelewesha makubaliano, wala haitaki kusitishwa kwa mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.