Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron azuru Jordan, vita kati ya Israel na Hamas kujadiliwa

Siku mbili baada ya kupitishwakwa sheria ya uhamiaji, Rais wa Ufaransa anafanya ziara nchini Jordan siku ya Alhamisi, Desemba 21 kama sehemu ya sherehe ya jadi ya Krismasi kwa wanajeshi. Pia atakutana na Mfalme Abdullah II wa Jordan. Fursa kwa Rais Macron kujadili na Mfalme wa Jordan vita kati ya Israel na Hamas, lakini pia hali ya kibinadamu ya wakazi wa Gaza.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Mfalme wa Jordan Abdullah II wakati wa ziara yake ya mwisho mjini Amman mnamo Oktoba 25, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Mfalme wa Jordan Abdullah II wakati wa ziara yake ya mwisho mjini Amman mnamo Oktoba 25, 2023. AP - Nicolas Messyasz
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Misri mwaka 2022, rais amechagua Jordan. Tayari alikuwa huko wiki chache zilizopita, lakini kutokana na habari za kimataifa, rais wa Ufaransa amechagua kurejea huko mwishoni mwa mwaka. Anakutana na Mfalme Abdullah II leo Alhamisi kujadili hali ya Mashariki ya Kati. Nchi hizo mbili zinafanya kazi pamoja kuufanya mji mkuu wa Jordan kuwa kitovu cha kibinadamu ili kupeleka misaada kwa wakazi wa Gaza.

Hii itakuwa "fursa ya kurejea kazi ambayo tunayo sawa na washirika wetu wa Jordan katika suala la misaada ya kibinadamu na matibabu kwa raia wa Gaza," imetangaza Ikulu ya Élysée. Ndege mbili za mizigo ya misaada ya kibinadamu inayokusudiwa kutolewa kwa raia katika Ukanda wa Gaza - ambazo zinatarajia kufanya safari zao leo Alhamisi hii na Desemba 26 - zitatua Amman.

Katika mkesha wa kuondoka kwake, rais wa Ufaransa alikumbuka msimamo wa Ufaransa juu ya mzozo kati ya Israeli na Hamas. "Kadiri wiki zinavyosonga, hatuwezi kuruhusu wazo lishikilie kwamba kupigana ipasavyo dhidi ya ugaidi kunaweza kumaanisha kuharibu kila kitu huko Gaza au kushambulia raia na kusababisha waathiriwa wa kiraia," alisema katika mahojiano na kituo cha France 5. "Hii ndiyo sababu, wakati tunatambua haki ya Israeli ya kujilinda wakati ikipigana dhidi ya ugaidi, tunadai ulinzi wa watu hawa na mapatano ya kusimamisha mapigano kwa sababu za kibinadamu," aliongeza.

Pia katika ajenda ya majadiliano ni muungano wa kimataifa dhidi ya Daesh, huku Jordan ikiwa mwenyeji wa kikosi cha operesheni ya Ufaransa ya Chammal katika kambi ya wanaanga ya Levant kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo. Kambi ambayo rais wa Ufaransa atatembelea baada ya mkutano huu na Mfalme wa Jordan kwa chakula cha jioni cha jadi cha Krismasi na askari na kutoa msaada wake na imani kwa majeshi katika eneo hili lenye umuhimu mkubwa.

Kwa jumla, wanajeshi 350, wengi wao kutoka jeshi la anga, watasherehekea Mkesha wa Mwaka Mpya pamoja na Emmanuel Macron siku ya Alhamisi hii jioni. Baada ya hotuba ya Mkuu wa Nchi, kutakuwa na chakula cha jioni kilichotayarishwa na mpishi wa jikoni kutoka ikulu ya  Élysée. Kwa sasa, bado haijajulikana kinachoandaliwa, lakini chokoleti kutoka kwa mpishi maarufu Alain Ducasse zitatolewa kwa askari.

Rais wa Ufaransa anatarajia kurejea Paris siku ya Ijumaa alasiri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.