Pata taarifa kuu

Marekani yatekeleza mashambulio dhidi waasi nchini Syria na Iraq

Nairobi – Jeshi la Marekani limeshambulia ngome 85 za kundi la waasi wenye silaha wanaodaiwa kuungwa mkono na serikali ya Iran nchini Syria na Iraq, na kusababisha vifo vya watu 16.

Iraq imeshtumu hatua hii ya jeshi la Marekani ikisema, mashambulio hayo yatakuwa na matokeo mabaya kwa ukanda huo
Iraq imeshtumu hatua hii ya jeshi la Marekani ikisema, mashambulio hayo yatakuwa na matokeo mabaya kwa ukanda huo AFP - DELIL SOULEIMAN
Matangazo ya kibiashara

Pentagon, ambao ndio uongozi wa jeshi la Marekani unasema umetekeleza mashambulio hayo kulipiza kisasi cha mashambulio ya ndege zisizokuwa na rubani, yaliyotekelezwa Jumapili iliyopita, kwenye kambi yake ya kijeshi nchini Lebanon na kuwauwa wanajeshi wake watatu.

Baada ya mashambulio hayo, rais wa Marekani Joe Biden amesema, majibu ya nchi yake yameanza na yataendelea hadi pale waasi hao watakavyoangamizwa.

Iraq imeshtumu hatua hii ya jeshi la Marekani ikisema, mashambulio hayo yatakuwa na matokeo mabaya kwa ukanda huo, huku Iran ikikanusha kuhusika na tukio la kuwalenga wanajeshi wake.

Katika mashambulio ya Jumamosi nchini Iraq, serikali jijini Baghdad imesema, raia wa kawaida ni miongoni mwa watu waliouawa.

Aidha, serikali ya Iran imelaani mashambulio hayo ya Marekani ikisema ni kukiuka sheria za kimataifa kuhusu uhuru wa nchi hizo mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.