Pata taarifa kuu

Palestine: Meli ya misaada imewasili Gaza

Nairobi – Meli iliyobeba dawa na vifaa vingine vya tiba, imewasili kwenye ukanda wa Gaza baada ya Qatar kwa msaada wa Ufaransa kusaidia kuwepo kwa maelewano ya kuruhusu kupita kwa shehena hiyo kati ya Israeli na kundi la Hamas.

Hatua hiyo imefanikishwa kwa uongozi wa Ufaransa na Qatar
Hatua hiyo imefanikishwa kwa uongozi wa Ufaransa na Qatar REUTERS - TYRONE SIU
Matangazo ya kibiashara

Wakati Meli ikiwasili, Shirika la Madaktari wasiokuwa na mipaka, wamesema, Jeshi la Israeli limeendeleza mashambulio mazito karibu na hospitali ya Nasser katika mji wa Khan Younis.

Mbali na wakaazi wa Gaza, kupata huduma hiyo ya tiba na msaada mwingine wa kibinadamu, mateka 45 waliotekwa na kundi la Hamas wanatarajiwa kunufaika.

Raia katika Ukanda wa Gaza wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu wa dawa na bidhaa nyengine ikiwemo maji
Raia katika Ukanda wa Gaza wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu wa dawa na bidhaa nyengine ikiwemo maji © MOFA QATAR / AFP

Msaada huu unakuja baada ya Shirika la afya duniani WHO kusema hali ya Gaza ni mbaya na wagonjwa wengi wanasubiri kufa kwa sababu ya kukosa dawa na wahudumu.

Wizara ya afya kwenye ukanda wa Gaza inasema mashambulio hayo yameacha maafa ya watu 11 na kuwaacha wengine wengi na majeraha.

Tangu kuanza kwa vita hivyo Oktoba mwaka uliopita, watu zaidi ya Elfu 24 wameuawa na wengine zaidi ya Elfu 61 wakiachwa na majeraha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.