Pata taarifa kuu

Israel imeonya kuwa eneo la Gaza si salama wakati huu mapigano yakiendelea

Nairobi – Israel imetekeleza mashambulio kusini mwa Gaza mapema Jumamosi, mashambulio yanayokuja wakati huu Umoja wa Mataifa ukionya kuwa eneo la Gaza kwa sasa sio salama kwa raia wa Palestina, vita vikiingia mwezi wa tatu sasa.

Mapigano hayo yalianza tarehe 7 ya mwezi Oktoba baada ya wapiganaji wa Hamas kutekeleza shambulio kusini mwa Israel
Mapigano hayo yalianza tarehe 7 ya mwezi Oktoba baada ya wapiganaji wa Hamas kutekeleza shambulio kusini mwa Israel REUTERS - AMIR COHEN
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yalianza tarehe 7 ya mwezi Oktoba baada ya wapiganaji wa Hamas kutekeleza shambulio kusini mwa Israel, hatua iliyopelekea Israel kujibu mashambulio hayo.

Makabiliano hayo yatakuwa yakiingia mwezi wa nne siku ya Jumapili ya wiki hii, matumaini ya kumalizika yakionekana kupungua kutokana na misimamo ya kila upande.

Vita hivyo vimewaathiri pakubwa raia wa Gaza ambayo wamepoteza makazi yao katika mashambulio, mzozo wa kibinadamu ukiripotiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa katika Ukanda huo.

Matumaini ya kumalizika kwa mapigano hayo yanaendelea kufifia pande hasimu zikionekana kutolegeza kamba
Matumaini ya kumalizika kwa mapigano hayo yanaendelea kufifia pande hasimu zikionekana kutolegeza kamba AP - Ariel Schalit

Mashambulio ya angani pia yameripotiwa mapema Jumamosi katika mji wa Kusini wa Rafah ambapo mamia kwa maelfu ya raia wa Gaza walikuwa wanapewa hifadhi baada ya kutoroka makazi yao kutokana na mashambulio.

Haya yanajiri wakati huu kundi la wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon likisema limerusha makombora kuelekea Israel kujibu mauaji ya naibu kiongozi wa kundi ka Hamas katika shambulio ambalo idara ya ulinzi ya Marekani.

Mapigano hayo yalianza tarehe 7 ya mwezi Oktoba baada ya wapiganaji wa Hamas kutekeleza shambulio kusini mwa Israel
Mapigano hayo yalianza tarehe 7 ya mwezi Oktoba baada ya wapiganaji wa Hamas kutekeleza shambulio kusini mwa Israel REUTERS - STRINGER

Naye waziri wa mambo ya nje ya Marekani Antony Blinken, anazuru nchini Uturuki ambapo anatarajiwa kujadili suala la Gaza na rais Recep Tayyip Erdogan.

Blinken pia atazuru mataifa kadhaa ya kiarabu kabla ya kuelekea nchini Israel na Ukiongo wa Magharibi wiki ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.