Gaza: Israeli yatoa mpango wake baada ya vita kukamilika
Naiorbi – Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant, ametangaza mapendekezo ya utawala wa ukanda wa Gaza, baada ya kumalizika kwa vita kati jeshi la nchi yake na kundi la Hamas.
Imechapishwa:
Cheza - 00:53
Miongoni mwa mipango inayowekwa na Israeli ni kuhakikisha kuwa, Gaza inaongozwa kwa kiwango kidogo na Wapalestina.
Kuhusu usalama, ukanda wote wa Gaza utakuwa chini ya Jeshi la Israeli, na kundi la Hamas halitaruhusiwa kuwepo.
Mapendekezo haya yanakuja, wakati huu jeshi la Israeli likiendeleza mashambulio ambayo kwa saa 24 zilizopita, mauaji ya watu yameendelea kushuhudiwa.
Wizara ya afya kwenye ukanda wa Gaza inasema watu 125 wameuawa kwa kipindi cha saa 24 zilizopita, wakati huu jeshi la Israeli likiapa kuendelea na operesheni dhidi ya kundi la Hamas katika vita ambavyo vimesbabisha vifo vya zaidia ya watu Elfu 22 mpaka sasa.
Vita vinaendelea wakati Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken anapotarajiwa kurejea kwenye ukanda huo ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Israeli na Palestina.