Jeshi la Israel ladai kugundua 'handaki kubwa zaidi' lililochimbwa chini ya Ukanda wa Gaza
Jeshi la Israel limedai siku ya Jumapili kuwa limegundua wakati wa mashambulizi yake "handaki kubwa zaidi" ambalo Hamas imechimba chini ya Ukanda wa Gaza na liko mita mia chache tu kutoka ardhi ya Israel. Mpiga picha wa shirka la habari la AFP ambaye ameidhinishwa kwenda katika eneo hilo amebainisha kuwa handaki hilo ni la ukubwa wa kutosha ambapo magari madogo yanaweza kupita.
Imechapishwa:
"Mtandao huu mkubwa wa handaki, ambao umegawanywa katika matawi kadhaa, unaenea kwa zaidi ya kilomita nne na unakuja mita 400 tu kutoka kivuko cha Erez" kati ya Israeli na Ukanda wa kaskazini wa Gaza, jeshi la Israeli limesema katika taarifa. Handaki hiyo ina mfumo wa bomba, umeme, uingizaji hewa, mifereji ya maji taka, mitandao ya mawasiliano na reli. Ardhi yake imetengenezwa kwa udongo uliopigwa na kuta zake zimetengenezwa kwa saruji iliyoimarishwa, isipokuwa kwenye kituo chake, kilichoimarishwa na silinda ya chuma takriban sentimita moja na nusu kwa kipenyo.
Wakati huo huo Malori 79 ya misaada ya kibinadamu yamepita Jumapili hii kupitia kituo cha mpaka cha Kerem Shalom, kilichofunguliwa leo.
Ili kupunguza uhaba wa chakula, maji, dawa na mafuta, tangu kuanza kwa vita na kuzingirwa kwa jumla kwa Ukanda wa Gaza ulioanzishwa mnamo Oktoba 9, Israeli ilianza kutoa msaada wa kibinadamu kutoka kivuko cha Kerem Shalom, kwenye mpaka na Misri.
Chanzo kutoka Shirika la Hilali Nyekundu la Misri, sawa na Msalaba Mwekundu, kimethibitisha kuwa lori 79 zilipitia kituo hiki siku ya Jumapili.