Pata taarifa kuu

Kuwait: Emir Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah afariki akiwa na umri wa miaka 86

Amir wa Kuwait, Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah, amefariki Jumamosi, Desemba 16, akiwa na umri wa miaka 86, imetangaza Kasri ya Amir, baada ya muhula wa miaka mitatu iliyokumbwa na migogoro ya kisiasa mara kwa mara katika uongozi wa nchi hii tajiri wa mafuta katika Ghuba.

Amir wa Kuwait, Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah (picha yetu), amefqriki Jumamosi, Desemba 16, akiwa na umri wa miaka 86, imetangaza Kasri ya Amir.
Amir wa Kuwait, Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah (picha yetu), amefqriki Jumamosi, Desemba 16, akiwa na umri wa miaka 86, imetangaza Kasri ya Amir. © AP - Jaber Abdulkhaleg
Matangazo ya kibiashara

"Kwa masikitiko makubwa, tunaomboleza kifo cha Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah, Amir wa Jimbo la Kuwait," imesema taarifa iliyotangazwa kwenye televisheni ya taifa ya Kuwait siku ya Jumamosi, Desemba 16. Hapo awali ilikuwa imekatiza programu zake na kutangaza aya za Qurani. Mnamo Novemba 2023, Sheikh Nawaf alilazwa hospitalini "kwa sababu ya tqtizo ya haraka ya kiafya," limeandika shirika la habari la serikali la KUNA, ambalo halikutoa maelezo ya ugonjwa wake.

Mgogoro wa kina

Baadaye alitangazwa kuwa hali yake ya afya inaendelea vizuri. Kwa kuzingatia umri wake, afya yake mara nyingi ilikuwa ya wasiwasi wakati wa utawala wake. Sheikh Nawaf alitawazwa kuwa mrithi wa taji mwaka wa 2006 na kaka yake wa kambo, Sheikh Sabah al-Ahmad Al-Sabah, na alichukua wadhifa wake baada ya kifo chake mnamo Septemba 2020 akiwa na umri wa miaka 91. Jimbo tajiri la mafuta katika Ghuba, Kuwait limetumbukia kwa miaka kadhaa katika mgogoro mkubwa kati ya mamlaka ya utendaji na sheria hali ambayo inadhoofisha matumaini ya mageuzi.

Sheikh Nawaf aliyezaliwa mwaka wa 1937, alikuwa mtoto wa tano wa Emir Sheikh Ahmad al-Jaber Al-Sabah (1921-1950). Alianza kazi yake ya kisiasa akiwa na umri wa miaka 25 kama gavana wa jimbo la Hawalli, kabla ya kuzindua kazi yake ya uwaziri. Kuingia madarakani, alilazimika kudhibiti mzozo wa kiuchumi uliosababishwa na kushuka kwa bei ya mafuta, ambayo ilisababisha kiwango cha uhuru cha nchi kupunguzwa na mashirika ya ukadiriaji mnamo 2020. Katika ngazi ya kidiplomasia, aliweka hali kama hiyo, akipendelea kutoanzisha uhusiano na Israel kama majirani zake Bahrain na Falme za Kiarabu wamefanya. Pia amedumisha uhusiano wa uwiano na Saudi Arabia na Iran, wapinzani wakubwa wa eneo hilo.

Kiongozi mwenye umri mdogo?

Mwana wa mfalme wa sasa, Mechaal al-Ahmad al-Jaber al-Sabah, kaka wa kambo wa Amir, ana umri wa miaka 83, na swali ambalo sasa linazuka ni ikiwa familia ya kifalme itachagua kiongozi mkuu zaidi. Kuwait, nchi ya kihafidhina ambapo mamlaka huru yamebakia kujilimbikizia mikononi mwa familia inayotawala ya Al-Sabah, hata hivyo ni nyumbani kwa Bunge lililo lenye ushawishi na lenye nguvu zaidi katika Ghuba.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.