Pata taarifa kuu

Shambulio katika hospitali Gaza: Umoja wa Afrika walaani mashambulizi ya Israel

Hospitali ya kanisa la Anglikani ya Al-Ahli Arabi, iliyoko katikati mwa jiji la Gaza, ilikumbwa na shambulio la anga Jumanne jioni, Oktoba 17. Wakati Israel na Hamas zikitupiana lawama, Umoja wa Afrika (AU) umeishutumu waziwazi Israel.

Mwanamke akikumbatia mto baada ya shambulio la anga katika Hospitali ya Al-Ahli Arabi, iliyoko katikati mwa jiji la Gaza, Oktoba 18, 2023.
Mwanamke akikumbatia mto baada ya shambulio la anga katika Hospitali ya Al-Ahli Arabi, iliyoko katikati mwa jiji la Gaza, Oktoba 18, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio dhidi ya hospitali ni "uhalifu wa kivita". Moussa Faki Mahamat alisema baada ya shambulio hilo siku ya Jumanne jioni. Katika mitandao ya kijamii, mwenyekiti wa Kamisheni ya AU amesema: "Hakuna maneno yanayoweza kueleza kikamilifu kulaani kwetu kwa shambulio la Israel katika hospitali moja huko Gaza, na kuua mamia ya watu."

Kwa mara nyingine tena, Umoja wa Afrika umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua. Siku moja baada ya shambulio la Hamas, Oktoba 7, Moussa Faki Mahamat alitoa wito kwa "madola makubwa ya dunia kuchukua majukumu yao ya kuweka amani na kudhamini haki za raia wa mataifa mawili".

Rais wa Misri pia amelaani shambulio hilo. Abdel Fattah Al-Sisi anazungumzia ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa: "Ninalaani vikali shambulio la anga lililofanywa na Israel katika hospitali ya Gaza." Shambulio hili la anga lilisababisha maandamano, hasa huko Tunis, mbele ya ubalozi wa Ufaransa. Huko Mauritania, waandamanaji walikusanyika mbele ya ubalozi wa Marekani, viongozi wametangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.