Pata taarifa kuu

Mahujaji wa Mauritius wakwama nchini Israeli

Nairobi – Wizara ya mambo ya kigeni ya Mauritius imesema mamia ya mahujaji kutoka kwenye taifa hilo, wamekwama mjini Bethlehem kufuatia mzozo wa hivi punde kati ya kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas na Israeli.

Mashirika kadhaa ya ndege yamesitisha safari zake katika maeneo ya Israeli na Palestina kutokana na mapigano kati ya pande hizo mbili
Mashirika kadhaa ya ndege yamesitisha safari zake katika maeneo ya Israeli na Palestina kutokana na mapigano kati ya pande hizo mbili AP - Adel Hana
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa walioripotiwa kukwama mjini Bethlehem ni wanachama 36 wa kundi hilo haswa kutoka parokia ya Kikatoliki ya St-Hélène katika jiji la pili kwa ukuwa la Curepipe.

Kwa mujibu wa Padre Gérard Mongelard, ambaye ni miongoni mwa mahujaji hao, waumini hao kwa sasa wako katika hali nzuri ambapo wanaishi katika hoteli moja mjini Bethlehem.

Walikuwa wanatarajiwa kuabiri ndege siku ya Jumapili jioni kuelekea nchini Uturuki kabla ya kurejea nyumbani baadae.

Mashirika kadhaa ya ndege yamesitisha safari za ndege kwenda nchini Israeli kutokana na makabiliano yanayoendelea kati ya kundi la Hamas na wapiganaji wa Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.