Pata taarifa kuu

Lebanon: Riad Salamé ajiuzulu kwenye wadhifa wake kama mkuu wa Benki Kuu

Riad Salamé ambaye anakabiliwa na mashitaka katika mahakama nchini Ufaransa na Ujerumani kwa ubadhirifu na utakatishaji wa fedha, anatarajia kujiuzyulu kwenye wadhifa wake maka mkuu wa Benki kuu Jumatatu Julai 31 bila mrithi wake kuteuliwa na serikali. Ombwe hili la uongozi kwa mkuu wa taasisi hiyo unazua wasiwasi mkubwa wakati nchi inapoelekea katika mwaka wake wa tano wa mdororo wa kiuchumi.

Gavana wa Benki kuu ya Lebanon Riad Salamé huko Beirut, Novemba 24, 2022.
Gavana wa Benki kuu ya Lebanon Riad Salamé huko Beirut, Novemba 24, 2022. © Banque centrale du Liban / via AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Beirut, Paul Khalifeh

Tofauti kubwa kati ya wadau wa kisiasa nchini Lebanon zimezuia kurefushwa, kwa visingizio mbalimbali, kwa mamlaka ya Riad Salamé, pamoja na uteuzi wa mrithi wake, ambaye kijadi ni kutoka dini ya Katoliki ya Maronite.

Kuondoka kwa mkuu wa Benki Kuu kunazua wasiwasi kuhusu uthabiti wa kifedha wa Lebanon, iliyokumbwa na mdororo wa kifedha ambao haujawahi kutokea kwa karibu miaka minne.

Kanuni ya Sarafu na Mikopo inaeleza kuwa endapo itatokea ombwe la uongozi wa Benki Kuu, naibu wa gavana wa kwanza kati ya wanne atachukua nafasi yake.

Lakini Wassim Mansouri, kutoka dhehebu la Kishia aliye karibu na Spika wa Bunge Nabih Berry, ametishia kujiuzulu na wenzake watatu ikiwa msururu wa hatua na mageuzi hayatapitishwa na Baraza la Wawakilishi: manaibu wa gavana wanaomba kutohusishwa ili wasiwajibike kwa uwezekano wa mdororo wa jumla wa kifedha.

Licha ya shinikizo, Wassim Mansouri na wenzake, hoja zao zimetupwa kapuni.

Kujiuzulu kwa manaibu hao gavana kumefutwa. Na hata kama baadhi ya manaibu wa gavana wanne wakiamua kuacha nyadhifa zao, watawajibika kuiendesha Benki Kuu kwa niaba ya mwendelezo wa utumishi wa umma.

Matukio yote yanazua hofu ya kutofanya kazi kwa taasisi kuu ya kifedha, ambayo inaweza kusababisha kushuka kwa thamani zaidi ya pauni ya Lebanon, ambayo tayari imepoteza 98% ya thamani yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.