Pata taarifa kuu

Iran na Saudi Arabia zaendelea kuimarisha uhusiano wao Beijing

Saudi Arabia na Iran zinachukua hatua nyingine katika kurekebisha uhusiano wao. Takriban wiki nne baada ya kutangazwa kwa makubaliano yaliyofadhiliwa na China, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili walikutana Alhamisi hii, Aprili 6 mjini Beijing. Riyadh na Tehran zinaonyesha nia yao ya kutekeleza makubaliano yaliyotiwa saini mwezi uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Umoja huo ulifikia kwa jitihada za  China mwezi uliopita, na mji mkuu wa China ndio ambao uliandaa mkutano huu. Mkuu wa diplomasia wa nchi mwenyeji ambaye alikamata mikono ya wenzake ili kuwaunganisha na kupelekea wawili hao kupeana mikono kwa mara ya kwanza.

Baada ya mazungumzo, viongozi wa kisiasa wa nchi walikutana. Alhamisi hii, mawaziri wa mambo ya nje walitia saini makubaliano ya kufunguliwa tena kwa uwakilishi wa kidiplomasia: balozi huko Riyadh na Tehran na balozi ndogo huko Jeddah na Mashhad. Na nchi hizo mbili zinasema hazitaki kuishia hapo. Katika taarifa ya pamoja, wanasema "kuwa tayari kuondoa vikwazo vyote kwa ajili ya upanuzi wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili".

Hatua zinazofuata zinapaswa kuwa kuanza tena kwa safari za ndege za moja kwa moja kati ya Iran na Saudi Arabia, upeanaji mpana wa visa na ziara za wajumbe rasmi na wawakilishi wa sekta ya biashara. Mfalme Salman tayari amemwalika rais wa Iran nchini Saudi Arabia, lakini hakuna tarehe iliyotangazwa.

Kwa mkutano huu, nchi hizo mbili zinaonyesha kuwa uhusiano unaendelea kuimarika. Na wanaonyesha matumaini, wakisema itaimarisha "usalama na utulivu" katika Mashariki ya Kati. Kurejeshwa kwa uhusiano huu kunaweza kufanya vizuri maendeleo kwenye faili la Yemen, ambapo nchi hizo mbili zinaunga mkono kambi zinazopingana, pamoja na kurejeshwa kwa Syria kwenye Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, ambayo mkutano wake ujao utafanyika nchini Saudi Arabia mwezi ujao. Lakini nchi hizo mbili zinadumisha masilahi na malengo yanayopingana. Na uimara wa ukaribu huu utategemea uzito wa kisiasa wa China na utapimwa tu kwa kipimo cha wakati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.