Pata taarifa kuu

Israel yaweka vikwazo vya kulipiza kisasi vya kifedha kwa Mamlaka ya Palestina

Katika mahojiano na Gazeti la Haaretz, Waziri Mkuu wa Palestina Mohammed Shtayyeh anazungumzia hatua za kulipiza kisasi za kifedha zilizowekwa na serikali ya Israel kwa Mamlaka ya Palestina. 

Waziri Mkuu wa Palestina Mohammad Shtayyeh, Agosti 18, 2022 mjini Ramallah.
Waziri Mkuu wa Palestina Mohammad Shtayyeh, Agosti 18, 2022 mjini Ramallah. © Mohamad Torokman / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Israel inawatuhumu maafisa wa Palestina kwa kuongoza mashambulizi ya kidiplomasia dhidi yake katika Umoja wa Mataifa kuhusu suala la uvamizi wa Israel katika maeneo ya Palestina.

"Vikwazo vya kifedha vya Israel vitasababisha kuanguka kwa Mamlaka ya Palestina," anaonya Waziri Mkuu wa Palestina Mohammed Shtayyeh katika safu za Gazeti la kila siku la Israel la Haaretz.

Kosa la Wapalestina? Baada ya kuzungumzia suala la ukoloni wa Israel katika Umoja wa Mataifa. Wapalestina pia wameitaka Mahakama ya Kimataifa ya Haki kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa kukaliwa kwa mabavu Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Jerusalem Mashariki. Azimio hilo lililopitishwa siku mbili baada ya kuapishwa kwa serikali mpya ya Israel, pia linaitaka Israel kukomesha ukoloni wa Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuitaka ICJ kuamua "matokeo ya kisheria ya kuendelea kwa Israel kukiuka haki ya raia wa Palestina" ya kujitawala".

Kwa nini kukasirisha serikali ya Israeli, ambayo ilijibu kwa uthabiti kupitia mlolongo wa vikwazo. Kikwazo zaidi kinahusu fedha za Mamlaka ya Palestina. Israel huumiza pale kuliko kuwa na donda, kwenye mfuko wa fedha. Serikali ya Israel, kama mamlaka inayokalia baadhi ya maeneo ya Palestina, inakusanya ushuru wa bidhaa na biashara zinazoingia katika maeneo ya Palestina, kiasi cha dola milioni 250 kwa mwezi. Kisha Israel inatoa theluthi mbili ya fedha hizo kwa Mamlaka ya Palestina. Serikali ya Israel sasa inaweka adhabu ya kifedha ya karibu dola milioni 40 kwa Wapalestina.

'Mamlaka ya Palestina yalengwa na vikwazo zaidi'

Hatua hizo "zinalenga kuweka wazi kuwa Israel italipisha gharama kwa jaribio lolote la kuidhuru katika jukwaa la kimataifa", kulingana na taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Eli Cohen.

Israel "Mamlaka ya Palestina inakabiliwa na vikwazo zaidi", anasikitika Mohamed Shtayyeh. Waziri Mkuu wa Palestina anaeleza: "Tunaishi chini ya uvamizi wa kikatili na Israeli inataka kutupiga marufuku kutoka kwa aina yoyote ya mapambano, hata yale ya amani". Anakumbusha kuwa Wapalestina kwa kiasi kikubwa wanategemea misaada ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.