Pata taarifa kuu

Miili ya wahamiaji 15 yapatikana katika pwani ya Syria

Siku ya Alhamisi, wahamiaji kadhaa wamepatikana wamekufa kaskazini magharibi mwa Syria. Watu wanane wamepatikana wakiwa hai.

Mji wa Tartus unapatikana upande wa magharibi wa Syria.
Mji wa Tartus unapatikana upande wa magharibi wa Syria. world factbook/wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya Syria imepata miili ya wahamiaji 15 kwenye bandari ya kaskazini-magharibi ya mji wa Tartous, wizara ya uchukuzi imesema siku ya Alhamisi, na kuongeza kuwa wengine wanane wameokolewa. "Watu 15 walipatikana wamekufa na manusura 8 walisafirishwa hadi hospitali ya al-Bassel huko Tartus," Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Syria Samer Kbrasli amesema katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Uchukuzi.

"Kulingana na walionusurika, boti hiyo iliondoka kwenye bandari ya Minié, kaskazini mwa Lebanon, siku chache zilizopita," ameongeza Samer Kbrasli, akibaini kwamba wahamiaji hao wanatoka mataifa kadhaa, bila maelezo zaidi.

Vikosi vya uokoaji vinajaribu kutafuta manusura wengine karibu na Tartus, ilmesema taarifa hiyo. Kutokana na mzozo mkubwa wa kiuchumi ambao Lebanon imetumbukia, wakimbizi wa Syria na Palestina, pamoja na Walebanon, wamejaribu katika miezi ya hivi karibuni kuvuka bahari ya Mediterania kwa boti kuelekea nchi za Ulaya, hususan kisiwa cha Cyprus, kilichoko kilomita 175 kutoka pwani ya Lebanon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.