Pata taarifa kuu

Shireen Abu Aqla: Mwanahabari wa Al Jazeera amezikwa mashariki mwa Jerusalem

Mwanahabari wa Televisheni ya Aljazeera Shireen Abu Akleh, raia wa Palestina na Marekani, aliyepigiwa risasi na kuuawa wiki hii akiripoti kuhusu operesheni ya wanajeshi wa Israel katika eneo la ukingo wa Magharibi, amezikwa leo Mashariki mwa mji wa Jerusalem huku waombolezaji wakikabiliana na wanajeshi wa Israeli.

Polisi wakiwa na jeneza la Shireen Abu Akleh mwanahabari wa  Al Jazeera.
Polisi wakiwa na jeneza la Shireen Abu Akleh mwanahabari wa Al Jazeera. REUTERS - MOHAMAD TOROKMAN
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya waombolezaji, wameshiriki katika mazishi ya mwanahabari huyo aliyekuwa na umri wa miaka 51.

Wakati mwili wake, ulipokuwa unapitishwa Mashariki mwa Jerusalem, wanajeshi wa Israeli waliwapiga wambolezaji waliokuwa wamebeba jeneza lililokuwa limembeba mwanahabari huyo.

Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas ambaye ameishtumu Israel kwa kuhusika na mauaji ya mwanahabari huyo, amesema atakwenda kwenye Mahakama ya Kimataifa ya ICC, kutafuta haki.

Mauaji yake, yamezua mvutano kati ya Palestina na Israeli, huku kila mmoja akimlaumu mwenzake. Kituo cha Aljazeera, kimesisistiza mwanahabri wake, alipigwa risasi kwa makusudi.

Uchunguzi wa awali wa Israel unaonesha kuwa, ni vigumu kufahamu ni nani hasa aliyehusika na mauaji ya mwanahabari huyo kwa kumpiga risasi.

Palestina ilikataa kushirikiana na Israeli kuchunguza mauaji hayo, huku Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa ukitaka ukweli kuwekwa wazi na wahusika kuchukuliwa hatua.

Mauawaji yake yamelaaniwa vikali kote duniani wakati huu mataifa ya Israeli na Palestina yakituhumiana kuhusu ni nani aliyehusika na kitendo hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.