Pata taarifa kuu

Rais wa falme za Kiarabu Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan amefariki

Rais wa nchi ya falme za kiaarabu Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan, amefariki akiwa na miaka 73 baada ya kuugua kwa muda mrefu, kifo chake kimedhibitishwa na kituo cha habari kinachomilikiwa na serikali.

Mohammed bin Zayed Al-Nahyan,Kiongozi wa nchi za falme za kiarabu.
Mohammed bin Zayed Al-Nahyan,Kiongozi wa nchi za falme za kiarabu. POOL/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Nafasi ya rais Sheikh Khalifa inatarajiwa kujazwa na kaka yake mfalme Mohammed bin Zayed, ambaye tayari anaonekana kuwa kiongozi wa UAE, sababu ya kifo chake haijatajwa.

Siku 40 za maombolezi zimetangazwa, ambapo bendera zitaperushwa nusu mlingoti wafanyikazi wa umma na wale wa sekta za kibnafsi wakitakiwa kupumzika kwa siku za kwanza tatu kama ishara ya kuonyesha heshima kwa hayati Sheikh Khalifa.

Sheikh Khalifa, aliingia madarakani kama kiongozi wa pili wa nchi hiyo ya miliki za kiarabu novemba 2004 akichukua nafasi ya babake kama kiongozi wa 16 wa Abu Dhabi.

Khalifa, hajaonekana katika umma tangu mwaka wa 2014 alipofanyiwa upasuaji baada ya kupooza japokuwa mchango wake mkubwa katika uwongozi uliendelea kuonekana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.