Pata taarifa kuu

Katibu mkuu wa UN amesikitishwa na mauwaji wa mwanahabari wa Al Jazeera.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa UN António Guterres, ameeleza kusikitishwa kwake na mauwaji ya mwanahabari wa shirika la habari la Al Jazeera Shireen Abu Aqla mwenye asili ya palestina na Marekani.

Shireen Abu Akleh,  mwanahabari Al-Jazeera
Shireen Abu Akleh, mwanahabari Al-Jazeera AP
Matangazo ya kibiashara

Guterres, ametaka uchunguzi huru na wa haraka kufanyika ilikubaini sababu za kifo cha mwanahabari huyo maarufu duniani.

Abu Aqla, 51, aliuwaua jumatano Mei 11 wakati akifuatilia operesheni ya wanajeshi wa Israeli katika eneo la West Bank, mzalishaji wa vipindi wa shirika akijeruhiwa kwenye tukio hilo ambalo limeendelea kukashifiwa.

Uwongozi wa Al Jazeera umekuwa ukisisitiza mwanahabari huyo aliliengwa kimakusudi na wanajeshi wa Israeli, madai ambao waziri mkuu wa Israeli Naftali Bennett amejitenga nayo akisema kuwa kuna uwezekano mkubwa Abu Aqla alilengwa na mpalestina aliyekuwa amejihami kwa bunduki.

Wito wa waziri mkuu Naftali Bennett, wakutaka kufanyika kwa uchunguzi wa pamoja kwenye tukio kati ya nchi yake na mamlaka ya palestina umekataliwa na Palestina.

Mahmoud Abbas, rais wa mamlaka ya Palestina naye kwa upande wake ametaka Israeli kuwajibishwa kibnafsi kwa tukio hilo.

Guteress katika taarifa yake amesistiza kuwa wanahabari hawapaswi kulengwa wakati wa machafuko akikashifu mashambulizi na mauwaji dhidi ya wapasha habari.

Wito wa Guteress unakuja wakati huu msemaji wa Ikulu ya White house Jen Psaki katika ukurasa wake Twitter akieleza kusikitishwa kwa wamarekani kutokana na mauwaji ya of Abu Aqla pamoja na mzalishaji wake wa vipindi.

Mwili wa Abu Aqla upo katika makao makuu ya mamlaka ya Palestina ambapo raia wanatarajiwa kutoa heshima zao mwisho kwa mwanahabari huyo, wanahabari wenzake wakimuenzi kama mtu aliyeelewa kazi yake.

Mamilioni ya watu wameonekana katika Ikulu ya rais wa Palestina Mahmoud Abbas wakitaka kushuhudia shughuli ya kutoa heshima za mwsiho kwa mwanahabari huyo, shughuli ambayo inaongozwa na maofisa wa usalama wa palestina.

Rais Mahmoud Abbas, katika hotuba yake amemtaja mwanahabari huyo kama mtu akiyefariki akijitolea kwa ajili ya taifa lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.