Pata taarifa kuu
UTURUKI-HAKI

Mahakama ya Uturuki yarejesha kesi ya Khashoggi kwa Saudi Arabia

Mahakama ya Uturuki imeamua Alhamisi, Aprili 7, kurejesha nchini Saudi Arabia faili ya mauaji ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari wa Saudi Arabaia aliyeuawa mwezi Oktoba 2018 katika majengo ya ubalozi mdogo wa Saudia huko Istanbul. Hatice Cengiz, mchumba wa Jamal Khashoggi, ametangaza kukata rufaa.

Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari wa Saudi Arabaia aliyeuawa mwezi Oktoba 2018 katika majengo ya ubalozi mdogo wa Saudia huko Istanbul.
Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari wa Saudi Arabaia aliyeuawa mwezi Oktoba 2018 katika majengo ya ubalozi mdogo wa Saudia huko Istanbul. REUTERS - OSMAN ORSAL
Matangazo ya kibiashara

"Tumeamua kuhamishia kesi hiyo hadi nchini Saudi Arabia," amesema jaji wa mahakama ya Istanbul ambapo kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa tangu mwezi Julai 2020, ikiwa na washtakiwa 26, wote raia wa Suadi Arabia.

"Hakuna mashtaka nchini Saudi Arabia. Mamlaka ya Saudia tayari imefunga kesi na kuamua kuwaachilia huru washukiwa wengi” , amesema Wakili Gokmen Baspinar, mwanasheria wa mchumba wa Jamal Khashoggi

Waziri wa Sheria wa Uturuki Bekir Bozdag alikuwa ametoa maoni mazuri kwa ombi la mwendesha mashtaka, ambaye alitaka "kufunga na kuhamisha faili" nchini Suadi Arabia. Mauaji ya Jamal Khashoggi, aliyeuawa na kukatwakatwa katika ubalozi mdogo wa Saudia, yanadhofisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya kikanda yenye waumini wengi wa dhehebu la Kisunni.

Uturuki ina nia ya kufufua uhusiano na Saudi Arabia

Lakini Uturuki, inayokabiliwa na mzozo wa kiuchumi, imekuwa ikitafuta maelewano na Saudi Arabia kwa miezi kadhaa. Kwa upande wa mmoja wa wanasheria wa mchumba wa Khashoggi, Wakili Gokmen Baspinar anasema, "uamuzi huu wa kuhamisha faili unakwenda kinyume na sheria" na "ni ukiukaji wa uhuru wa Uturuki". "Hakuna mashtaka nchini Saudi Arabia. Mamlaka ya Saudia tayari imefunga kesi na kuamua kuwaachilia huru washukiwa wengi," amekumbusha wakili huyo, akiongeza kwamba amewasilisha "rufaa mbele ya mahakama ya utawala ya Ankara dhidi ya uamuzi wa wizara". Kwa mujibu wa mwanasheria mwingine, Wakili Ali Ceylan, uamuzi huu ni sawa na "kumtupa mwana-kondoo katika mdomo wa mbwa mwitu".

Mchumba wa Jamal Khashoggi, Hatice Cengiz, ambaye alikuwa akimsubiri Jamal Khashoggi nje ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia ambako alikuja kuchukua vyeti siku ya mauaji, amekata rufaa. "Hapa Hatutawaliwi na familia kama Saudi Arabia. Tuna mfumo wa mahakama ambao unajibu malalamiko ya raia: kwa hivyo, tutakata rufaa, "amewaambia waandishi wa habari wakati alipokuwa akitoka katika mahakama ya Istanbul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.