Pata taarifa kuu
UFARANSA-HAKI

Mauaji ya Khashoggi: Mshukiwa aliyekamatwa Ufaransa sio mshukiwa anayetafutwa na Uturuki

Msaudia aliyekamatwa Jumanne nchini Ufaransa, ambaye alishukiwa kuwa katika kikosi kilichofanya mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi mwaka 2018, sio mshukiwa anayesakwa na Uturuki na ameachiliwa, mwendesha mashitaka wa jamhuri jijini Paris ametangaza.

Jamal Khashoggi aliuawa mwaka 2018 katika ubalozi wa Saudi Arabia, huko Istanbul.
Jamal Khashoggi aliuawa mwaka 2018 katika ubalozi wa Saudi Arabia, huko Istanbul. MOHAMMED AL-SHAIKH AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mwanasheria Mkuu wa Paris anaonyesha kuwa uchunguzui umethibitisha kwamba raia wa Saudia aliyekamatwa huko Roissy Jumanne asubuhi hakuwa mshukiwa anayetafutwa na Uturuki katika kesi ya Khashoggi. Ni jina linalofanana na la mshtumiwa.

Mwanamme huyo, aliyekuwa na pasipoti yenye jina la Khaled Alotaibi alikamatwa na polisi wa ulinzi wa mipaka wa Ufaransa katika uwanja mkuu wa ndege mjini Paris hapo jana wakati akijiandaa kupanda ndege kuelekea Riyadh.

Mtu anayejulikana kama Khaled Alotaibi ni mmoja wa washukiwa 26 walioshitakiwa bila kuweko mahakamani nchini Uturuki kwa kuwa sehemu ya kikosi kilichofanya mauaji ya Khashoggi katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul.

Pia amewekewa vikwazo na Wizara ya Fedha ya Marekani kwa kuhusika kwake na mauaji hayo. Ubalozi wa Saudia mjini Paris umesema mtu huyo aliyekamatwa hahusiki kwa namna yoyote katika kesi hiyo inayozungumziwa, na kutaka aachiwe mara moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.