Pata taarifa kuu
UINGEREZA-IRAN

Uingereza yaendelea kuihusisha Iran katika shambulizi la meli ya Mercer Street

Uingereza, pamoja na Romania na Liberia, wameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumanne wiki kuwa "kuna uwezekano mkubwa" Iran kuhusika katika shambulio dhidi ya meli ya mafuta ya Mercer Street, wiki iliyopita, kwa kutumia ndege moja au nyingi zisizo kuwa na rubani. 

Tehran imekanusha kuhusika kwa shambulio hilo wiki iliyopita hidi ya meli ya mafuta ya Mercer Street, inayosimamiwa na kampuni ya Israeli. Wafanyikazi wawili - Mwingereza na Mromania - waliuawa katika shambulio hilo.
Tehran imekanusha kuhusika kwa shambulio hilo wiki iliyopita hidi ya meli ya mafuta ya Mercer Street, inayosimamiwa na kampuni ya Israeli. Wafanyikazi wawili - Mwingereza na Mromania - waliuawa katika shambulio hilo. Karim SAHIB AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika barua kwa wanachama 15 wa baraza hilo, kulingana na shirika la habari REUTERS, nchi hizo tatu zimeaandika kwamba shambulio hilo "lilisababisha hatari kwa usalama wa usafirishaji wa mizigo katika ngazi ya kimataifa na ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa."

"Kitendo hiki lazima kilaaniwe na jamii ya kimataifa," nchi hizo tatu zimeongeza katika waraka huo.

Tehran imekanusha kuhusika kwa shambulio hilo wiki iliyopita hidi ya meli ya mafuta ya Mercer Street, inayosimamiwa na kampuni ya Israeli. Wafanyikazi wawili - Mwingereza na Mromania - waliuawa katika shambulio hilo.

Kulingana na wanadiplomasia, Uingereza inapanga kuzungumzia suala hilo katika siku zijazo wakati wa mkutano wa faragha wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.