Pata taarifa kuu
IRAN

Ebrahim Raïssi aidhinishwa kuwa rais wa Iran

Ebrahim Raïssi, moja wa maafisa wenye msimamo mkali nchini Iran ametawazwa kuwa rais wa nchi hiyo Jumanne hii Agosti 3 na atakuwa na kibarua kikubwa kwa kufufua uchumi uliothiriwa na vikwazo vya Marekani na mgogoro wa afya uliosababishwa na gonjwa la COVID-19, na kuanzisha tena mazungumzo ili kuokoa makubaliano ya kimataifa kuhusu mpango nyuklia ya wa Iran.

Rais mteule wa Iran Ebrahim Raïssi, wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa mwezi Juni, Tehran, Juni 21, 2021.
Rais mteule wa Iran Ebrahim Raïssi, wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa mwezi Juni, Tehran, Juni 21, 2021. AFP - ATTA KENARE
Matangazo ya kibiashara

Ebrahim Raïssi, ambaye ni mshindi wa uchaguzi wa urais wa mwezi Juni, anamrithi Hassan Rohani (mwenye msimamo wa wastan), ambaye mwaka wa 2015 alihitimisha makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na nchi zenye nguvu duniani, baada ya mvutano wa miaka kadhaa.

Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Mahakama, Bwana Raïssi, 60, anaanza rasmi kipindi chake cha miaka minne baada ya uchaguzi wake kuidhinishwa na Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei.

"Kulingana na matakwa ya wananchi, ninamuidhinisha mtu mwenye busara, mpambanaji, mzoefu na maarufu Ebrahim Raïssi kuwa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran," ameandika Kiongozi Mkuu katika agizo lililoosomwa na msaadizi wake mkuu.

Ayatollah Khamenei anatarajiwa kuhutubia taifa baada ya hotuba fupi ya rais mpya, katika sherehe ambapo, kwa sababu ya janga la Covid-19,  idadi ndogo ya maafisa ndio walioalikwa.

Bwana Raïssi ataapishwa Alhamisi mbele ya Bunge, ambapo atawasilisha majina ya wajumbe katika nafasi za mawaziri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.