Iran yashtumiwa kwa kuanza kurutubisha madini ua Uranium
Marekani na mataifa ya Ulaya yamelaani hatua ya Iran kuanza tena urutubishaji wa madini ya Uranium kwa asilimia 20 kinyume na makubaliano ya Kimataifa yaliyokubaliwa mwaka 2015.
Imechapishwa:
Kituo cha Kimataifa kinachoshughulia nishati ya Atomic, kinaonya kuwa hatua hiyo ya Iran inahatarisha mazungumzo ambayo yamekuwa yakiendelea kujaribu kupata suluhu ya suala hilo.
Ned Price, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje wa Marekani, amesema uongozi wa rais Joe Biden unasikitishwa na mwenendo wa Iran.
Inazua wasiwasi kuwa Iran inachagua kutosimamia utekelezwaji wa mkataba uliokubaliwa kwa majarbio inayofanya, hakika hii inasikitisha sana, tunapenda kutoa wito kwa Iran kuacha kurudi nyuma na kurejea kwenye mazungumzo huko Vienna ili kumalizia kazi iliyoanza mwezi Aprili, mazungumzo ambayo yamefikia hatua ya sita.
Mataifa ya Magharibi yanahofia kuwa, iwapo Iran itafanikiwa katika mpango wake, itakuwa inakaribia kutengeneza silaha za nyuklia na hivyo kutishia usalama wa dunia.
Tangu rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aiondoe nchi yake kwenye mpango wa pamoja wa makubaliano kuhusu mradi huu (JCPOA) mwaka 2018, Iran imeendelea kwenda kinyume na makubaliano ya kusitisha urutubishaji wa uranium.