Pata taarifa kuu
ISRAELI-SIASA

Israeli: Bunge kupigia kura muungano mpya Juni 13

Kura ya imani kwa serikali mpya ya Israeli, ambayo inaweza kumwondoa madarakani Waziri Mkuu aliyeko madarakani Benjamin Netanyahu, itafanyika ifikapo Jumapili Juni 13, Spika wa Bunge Yariv Levin amesema, bila kutoa maelezo zaidi.

Naftali Bennett, kutoka chama cha Yamina, atoa taarifa katika Bunge la Israeli, huko Knesset, Juni 6, 2021.
Naftali Bennett, kutoka chama cha Yamina, atoa taarifa katika Bunge la Israeli, huko Knesset, Juni 6, 2021. AP - Yonatan Sindel
Matangazo ya kibiashara

Naftali Bennett, ambaye amempa msaada kiongozi wa upinzani wa mreno wa kati, Yarist Lapid, na anayetajwa kuwa waziri mkuu mteule, amemsihi Benjamin Netanyahu, aliyeko madarakani tangu 2009, "aachilie ngazi".

Wawili hawa wanaoonoza muungano huo mpya, unaoundwa na vyama tofauti vya kiitikadi lakini wanaotaka kumtoa Benjamin Netanyahu mamlakani, wanasema wana uwezo wa kuunda serikali mpya na wamemjulisha Spika wa Bune Yariv Levin, na vile vile Rais wa Israel Reuven Rivlin.

Naftali Bennett amemtolea wito Spika wa Bunge, mshirika wa karibu nwa Benjamin Netanyahu, kuitisha kikao cha Bunge kwa minajili ya kupigia kura ya kuwa na imani na muunano mpya siku ya Jumatano ili serikali mpya iapishwe.

Yariv Levin, kutoka chama cha Likud, kama Waziri Mkuu Benjamin Netranyahu, amesema kwamba kulingana na tarehe ya mwisho iliyowekwa na sheria, kura hii inaweza kufanyika kabla ya Juni 14. Muda huu mdogo unampa Benjamin Netanyahu nafasi ya ziada ya kumaliza mradi wa muungano mpya.

Ikiwa muungano hu hautapata wingi wa kura bungeni, uchauzi wa tano utafitishwa chini ya miaka miwili nchini Israeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.