Pata taarifa kuu
ISRAELI-SIASA

Netanyahu: Muungano mpya ni hatari kwa Israel

Waziri Mkuu wa Israeli anayemaliza muda wake Benjamin Netanyahu amekosoa vikali makubaliano yaliyofikiwa kati ya vyama tofauti vya kisiasa ili kumwondoa mamlakani, nafasi ambayo amekuwa akishikilia tangu mwaka 2009.

Waziri Mkuu wa Israeli anayemaliza muda wake Benjamin Netanyahu.
Waziri Mkuu wa Israeli anayemaliza muda wake Benjamin Netanyahu. YONATAN SINDEL POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Akijieleza kupitia mandao wa Twitter, amesema: "Wabunge wote waliochaguliwa na kura za mrengo wa kulia lazima wapinge serikali hii hatari ya mrengo wa kushoto."

Hii ni taarifa yake ya kwanza kwa umma tangu kiongozi wa upinzaji Yair Lapid aliposema yuko katika nafasi nzuri ya kuunda serikali mpya ya muungano.

Karibu dakika 35 kabla ya tarehe ya mwisho iliyowekwa kwake Jumatano usiku wa manane (22:00 GMT), Yair Lapid, kutoka mrengo wa kati, amesema katika barua pepe kwa mkuu wa nchi, Reuven Rivlin: "Nimefurahiya kukujulisha kuwa nimefaulu kwa kuunda serikali ".

Wanasiasa hao wa upinzani wamekubaliana kuwa nafasi ya Waziri Mkuu miongoni mwao itakuwa kwa mzunguko, na kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia cha Yamina, Naftali Bennet, ndiye ataanza kushika madaraka hayo kabla ya kumkabidhi Bwana Yair Lapid.

Kabla ya kuanza kazi, serikali hii mpya, itapigiwa kura na wabunge ili kuidhinishwa.

Iwapo serikali hiyo itashindwa kupata uungwaji mkono wa wabunge 120, basi itawazalimu Waisraeli wapige tena kura, utakuwa ni uchaguzi wa tano ndani ya miaka miwili ili kupata serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.