Pata taarifa kuu
PALESTINA

Palestina kufanya uchaguzi wa urais wa kihistoria Julai 31

Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas ametangaza kuwa nchi yake itafanya uchaguzi wa kihistoria mwaka huu kumchagua rais mpya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 15.

Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina  Mahmoud Abbas
Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas AP Photo/Majdi Mohammed
Matangazo ya kibiashara

Abbas amebaini kwamba uchaguzi wa urais umepangwa kufanyika Julai 31 na uchaguzi wa wabunge utafanyika Mei 22. Wapiga kura wa Ukingo wa Magharibi, Ukanda wa Gaza na Jerusalem Mashariki wanaruhusiwa kushiriki katika uchaguzi huo.

Kauli hiyo inakuja wakati nchi hiyo inaendelea kuwa na mvutano na jirani yake Israeli, huku utovu wa usalama ukiendelea kuripotiwa katika maeneo ya mpakani kati ya nchi hizi mbili.

Uchaguzi wa mwisho wa urais Palestina ulifanyika mwaka 2005, huku uchaguzi wa bunge ukifanyika mwaka 2006.

Uchaguzi umekuwa ukipangwa mara kadhaa katika miaka michache iliyopita, lakini hakuna agizo la rais lililowahi kusainiwa. Chama cha Abbas, Fatah ambacho kinatawala Mamlaka ya Palestina kwenye Ukingo wa Magharibi na kundi la Hamas linaoidhibiti Gaza kwa miaka kadhaa wameonesha nia ya kuandaa uchaguzi kwa ajili ya Wapalestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.