Pata taarifa kuu
LEBANON-UFARANSA-SIASA-USALAMA

Rais Macron kuzungumzia kuhusu Lebanon Jumapili jioni

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajia kuzungumzia kuhusu hali ya kisiasa nchini Lebanon leo Jumapili jioni kwenye mkutano na waandishi wa habari, kufuatia tangazo la Waziri Mkuu wa Lebanon ambaye amejiondoa katika mpango wa kuunda serikali mpya, ikulu ya rais imetangaza.

Waziri Mkuu mpya wa Lebanon, Moustapha Adib, anazungumza na waandishi wa habari katika ikulu ya rais, baada ya kuteuliwa kwake, Agosti 31, 2020.
Waziri Mkuu mpya wa Lebanon, Moustapha Adib, anazungumza na waandishi wa habari katika ikulu ya rais, baada ya kuteuliwa kwake, Agosti 31, 2020. REUTERS/Mohamed Azakir
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa, ambaye mikutano na waandishi wa habari katika ikulu ya rais ni nadra sana, anataka kuingilia kati baada ya kushindwa kwa vyama vya siasa vya Lebanon kuunda serikali katikati ya mwezi Septemba, kama iliyokuwa iliafikiwa mbele yake katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

Waziri Mkuu Mustapha Adib ameachana na juhudi za kuunda serikali mpya kutokana matakwa ya mabadiliko kutoka kwa walio wengi.

Ripoti mbalimbali zinasema ni kutokana na ugumu wa upande wa Shia unaohitaji kushikilia wizara ya fedha na wizara ya juu ndani ya baraza la mawaziri.

Adib ambaye awali alikuwa balozi wa Lebanon nchini Ujerumani aliteuliwa kuwa waziri mkuu mnamo Agosti 31, na kutwishwa jukumu la kuunda serikali baada ya uingiliaji kati wa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Serikali hiyo ingefuata mpango uliopendekezwa na Ufaransa kwa ajili ya kuiondoa Lebanon katika mkwamo wa kisiasa, kwa kupiga vita ubadhirifu na kutekeleza mageuzi ambayo yangevutia msaada wa kimataifa wenye thamani ya mabilioni ya dola, ili kuunusuru uchumi wa Lebanon unaokabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni.

Hali mbaya ya uchumi wa Lebanon ilizidi makali baada ya mripuko mkubwa kwenye bandari ya Beirut wa Agosti 4, 2020, ambao uliharibu kabisa sehemu kubwa ya mji huo mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.