Pata taarifa kuu

Palestina yataka mkutano wa Umoja wa Mataifa, msimamo wa Trump wakosolewa

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ametoa wito kwa Umoja wa mataifa kufanyika mkutano wa kimataifa juu ya mzozo wa Israeli na Palestina mapema mwaka 2021.

Mahmoud Abbas amekosoa vikali makubaliano ya kihistoria yaliyofikiwa wiki za hivi karibuni nkati ya Israeli na Falme za Kiarabu na Bahrain, chini ya mwavuli wa ya Rais wa Marekani.
Mahmoud Abbas amekosoa vikali makubaliano ya kihistoria yaliyofikiwa wiki za hivi karibuni nkati ya Israeli na Falme za Kiarabu na Bahrain, chini ya mwavuli wa ya Rais wa Marekani. ABBAS MOMANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Bw. anasema ana matumaini ya kuepo kwa mwanzo mpya baada ya uchaguzi wa urais nchini Marekani, akishtumu utawala wa Trump kuwa na msimamo wa kuegemea.

"Natoa wito kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuanza maandalizi" ya "mkutano wa kimataifa mapema mwaka ujao," Mahmoud Abbas amesema wakati wa hotuba yake ya video kwenye mkutano mkuu wa Umoja aw Mataifa wa kila mwaka.

"Mkutano huu lazima uwe na mamlaka yote muhimu kuzindua mchakato wa amani wa dhati kwa msingi wa sheria za kimataifa", ili "kumaliza mpango wa Israeli wa kukalia kimabavu maeneo ya Palestina", Mahmoud Abbas amebaini.

Amekosoa vikali makubaliano ya kihistoria yaliyofikiwa wiki za hivi karibuni nkati ya Israeli na Falme za Kiarabu na Bahrain, chini ya mwavuli wa ya Rais wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.