Pata taarifa kuu
LEBANON-USALAMA-MSAADA

Raia wa Lebanon watoa misaada kwa minajili ya waathiriwa wa milipuko ya Beirut

Msaada wa kimataifa umeanza kuwasili nchini Lebanon, siku mbili baada ya milipuko miwili kubwa ambayo iligharimu maisha ya watu zaidi ya 100 na maelfu kujeruhiwa.

Watu wanaojitolea kusafisha barabara baada ya milipuko ya Jumanne katika eneo la bandari la Beirut, Lebanon, Agosti 5, 2020.
Watu wanaojitolea kusafisha barabara baada ya milipuko ya Jumanne katika eneo la bandari la Beirut, Lebanon, Agosti 5, 2020. REUTERS/Mohamed Azakir
Matangazo ya kibiashara

Rais Emmanuel Macron amefanya ziara nchini Lebanon na sasa yuko mjini Beirut. Amekutana na mwenzake wa Lebanon Michel Aoun na Waziri Mkuu Hassan Diab. Ufaransa imethibitisha kupelekwa kwa ndege tatu za kijeshi kwa ajili ya msaada. Wakati huo huo, raia wa Lebanon wameendelea kutoa mshikamano wao ili kusaidia mamia ya maelfu ya waathariwa.

Hayo yanajiri wakati serikali ya Lebanon imetangaza hali ya dharura kwa kipindi cha wiki mbili katika mji wa Beirut, baada ya milipuko miwili iliyotokea katika bandari ya mjini Beirut iliyosababisha vifo vya watu wengi.

Akizungumza mapema katika hotuba iliyorushwa na televisheni wakati wa kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri, rais Aoun amesema wamedhamiria kuchunguza na kufichua kile kilichotokea na kisha kuwaadhibu wale walihusika.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa uzembe wa miaka mingi wa kuhifadhi kemikali hatari katika ghala moja karibu na bandari mjini Beirut ndiyo chanzo cha milipuko hiyo iliogharimu laisha ya watu 100 na kujeruhi maelfu wengine.

Wakati huo huo ofisi ya mwendesha mashtaka ya Paris imesema kuwa watu wasiopungua 21, raia wa Ufaransa wamejeruhiwa katika milipuko hiyo katika bandari ya Beirut na kutangaza kwamba imefungua uchunguzi kuhusu "majeraha ya bila kukusudia".

Ripoti ya hivi karibuni ya Shirika la Msalaba Mwekundu inaripoti kuwa watu wasiopungua 113 wamepoteza maisha katika tukio hilo na zaidi ya 4,000 wamejeruhiwa.

Kulingana na ripoti ya awali, raia 21 wa Ufaransa ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa, ofisi ya mashtaka imebaini katika taarifa yake.

Mataifa ya ghuba yamekuwa ya kwanza kutuma msaada baada ya Qatar kupakia shehena ya vitanda vya hospitali, majenereta na shuka inayotarajiwa kuwasili baadae leo mjini Beirut.

Umoja wa Ulaya, Uturuki na mataifa mengine mengi yametangaza kutuma msaada wa kitaalamu na kiutu kwenda Lebanon kusaidia juhudi za uokoaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.