Pata taarifa kuu
LEBANON-USALAMA

Lebanon: Hali ya dharura yatangazwa Beirut kwa kipindi cha wiki mbili

Serikali ya Lebanon imetangaza hali ya dharura kwa kipindi cha wiki mbili katika mji wa Beirut, baada ya milipuko miwili iliyotokea katika bandari mjini Beirut iliyosababisha vifo vya watu wengi.

Timu maalumu iliyotumwa na Jamhuri ya Czech inajiandaa kwenda Beirut Agosti 5.
Timu maalumu iliyotumwa na Jamhuri ya Czech inajiandaa kwenda Beirut Agosti 5. REUTERS/David W Cerny
Matangazo ya kibiashara

Serikali imetangaza "hali ya dharura katika mji wa Beirut kwa kupindi cha wiki mbili", Waziri wa Habari, Manal Abdel Samad ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari.

Akizungumza mapema katika hotuba iliyorushwa na televisheni wakati wa kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri, rais Aoun amesema wamedhamiria kuchunguza na kufichua kile kilichotokea na kisha kuwaadhibu wale walihusika.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa uzembe wa miaka mingi wa kuhifadhi kemikali hatari katika ghala moja karibu na bandari mjini Beirut ndiyo chanzo cha milipuko hiyo iliogharimu laisha ya watu 100 na kujeruhi maelfu wengine.

Wakati huo huo ofisi ya mwendesha mashtaka ya Paris imesema kuwa watu wasiopungua 21, raia wa Ufaransa wamejeruhiwa katika milipuko hiyo katika bandari ya Beirut na kutangaza kwamba imefungua uchunguzi kuhusu "majeraha ya bila kukusudia".

Ripoti ya hivi karibuni ya Shirika la Msalaba Mwekundu inaripoti kuwa watu wasiopungua 113 wamepoteza maisha katika tukio hilo na zaidi ya 4,000 wamejeruhiwa.

Kulingana na ripoti ya awali, raia 21 wa Ufaransa ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa, ofisi ya mashtaka imebaini katika taarifa yake.

Mataifa ya ghuba yamekuwa ya kwanza kutuma msaada baada ya Qatar kupakia shehena ya vitanda vya hospitali, majenereta na shuka inayotarajiwa kuwasili baadae leo mjini Beirut.

Umoja wa Ulaya, Uturuki na mataifa mengine mengi yametangaza kutuma msaada wa kitaalamu na kiutu kwenda Lebanon kusaidia juhudi za uokoaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.