Pata taarifa kuu
LEBANON-USALAMA

Rais wa Lebanon atiwa wasiwasi na hali ya 'vita vya wenyewe kwa wenyewe'

Rais wa Lebanon Michel Aoun ameelezea kuhusu "mazingira ya vita vya wenyewe kwa wenyewe" vinayoikabili nchi yake, siku chache baada yamaandamano ya kiraia ya hivi karibuni yaliyofanyika hasa huko Beirut.

Rais wa Lebanon Michel Aoun wakati wa hotuba yake kwa taifa kutoka Ikulu ya rais ya Baabda, Oktoba 24, 2019.
Rais wa Lebanon Michel Aoun wakati wa hotuba yake kwa taifa kutoka Ikulu ya rais ya Baabda, Oktoba 24, 2019. Dalati Nohra/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Rais Michel Aoun amesema ana wasiwasi na mamabo yanayofanywa yenye lengo la kuchochea mivutano kati ya jamii wakati nchi hiyo inaendelea kukumbwa na mdororo wa kiuchumi.

Rais wa Lebanon ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano kwa niaba ya mazungumzo ya kitaifa, tukio lililosusiwa na Waziri Mkuu wa zamani kutoka dhehebu la Kisunni Saad Hariri na wakuu wengine wa zamani wa serikali ambao katika siku za hivi karibuni walisema kushiriki mazungumzo hayo ni kama kupoteza muda.

"Ninaelezea wasiwasi mkubwa niao kufuatia mazingira ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ninayoona," Michel Aoun amesema baada ya makabiliano mapema mwezi Mei huko Beirut kati ya Washia

na Wakristo, kwa upande mmoja, na Washia na Wasunni, kwa upande mwingine.

Karibu nusu ya raia wa Lebanon wanaishi katika umaskini mkubwa kulingana na Benki ya Dunia; Lebaon inakabiliwa na mdororo mbaya zaidi wa kiuchumi tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya 1975-1990.

Hali hiyo imezidi kuzorota kufuatia maandamano yaliyoanza mwezi Oktoba yanayolenga wanasiasa na ufisadi. Tangu wakati huo, sarafu ya Lebanon imepoteza asilimia 75 ya thamani yake, bei ya bidhaa za chakula imeongezeka na kampuni nyingi zimelazimika kufunga milango.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.