Pata taarifa kuu
PAKISTANI-USALAMA

Pakistan: Sita wauawa katika shambulio la watu wenye silaha Karachi

Angalau watu sita wameuawa, ikiwa ni pamoja na afisa wa polisi, wakati watu wanne wenye silaha walipojaribu kuingia kwenye soko la Hisa la Karachi (Kusini), mji mkuu wa kifedha wa Pakistani.

Kikosi cha jeshi la Pakistani, huko Karachi, Pakistan Novemba 23, 2018.
Kikosi cha jeshi la Pakistani, huko Karachi, Pakistan Novemba 23, 2018. REUTERS/Akhtar Soomro
Matangazo ya kibiashara

Kundi la wanaharakati kutoka mkoa jirani wa Balochistan wanaotaka eneo hilo kujitenga limedai kuhusika na shambulio hilo.

Washambuliaji, ambao angalau wawili walikuwa wamevalia nguo za kimagharibi, kulingana na picha za miili yao zilizopigwa na shirika la habari la AFP, walijaribu kuingia, kabla ya kurusha guruneti na kufyatua risasi, Amesema Ghulam Nabi Memon, mkuu wa polisi katika mji wa Karachi.

"Karibu saa 10:00 asubuhi, walijaribu kuingia ndani ya jengo hilo. Lakini walipofika mbele ya" jengo hilo waligunduliwa, amesema Ahmed Chinoy, mjumbe wa kamati kuu ya Soko la Hisa la Pakistan, ambayo ni inajumuisha maeneo ya Karachi, Lahore na Islamabad.

"Walinzi wanne na raia mmoja wameuawa," pamoja na afisa wa polisi, katika "shambulio hilo la kigaidi", polisi imesema katika taarifa, huku ikibaini kuwa kuna maafisa watatu wa polisi ambao wamejeruhiwa.

Shirika la Edhi, shirika kuu la misaada huko Karachi, kwa upande wake limebaini kwamba watu saba wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa, kiongozi wa shirika hilo Faisal Edhi ameliambia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.