Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-USHIRIKIANO

Antonio Guterres aisihi Israeli kusitisha mpango wa kunyakuwa Ukingo wa Magharibi

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito kwa Israeli kuachana na mipango yake ya kulifanya eneo la Ukingo wa Magharibi kuwa moja ya sehemu ya nchi hiyo na kuendelea na ujenzi wa makazi ya Wayahudi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Septemba 18, 2019.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Septemba 18, 2019. ©REUTERS/Carlo Allegri
Matangazo ya kibiashara

"Kama mpango huo, utatekelezwa, inaweza kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa, na hivyo itahatarisha juhudi za kupata suluhisho kati ya nchi hizo mbili na itapunguza uwezekano wa kuanza tena kwa mazungumzo," Antonio Guterres amesema mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

"Ninatoa wito kwa serikali ya Israeli kuachana na mipango yake ya kudhibiti eneo la Ukanda wa Magharibi," ameongeza.

Guterres amesema katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press (AP) kuwa Umoja wa mataifa umekuwa ukitoa mara kwa mara ujumbe kuwa unyakuaji huo hautakuwa tu dhidi ya sheria za kimataifa lakini utakuwa tukio kubwa la kuyumbisha usalama wa Mashariki ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.