Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAELI-UNSC-USHIRIKIANO-USALAMA

Umoja wa Mataifa waionya Israeli juu ya mpango wa kuunganisha ardhi za Ukingo wa Magharibi

Jumatano Mei 20, Mahmoud Abbas, rais wa Mamlaka ya Palestina, alionya kwamba anaweza kusitisha ushirikiano wa kiusalama na Israeli. Na hiyo inakuja, siku tatu baada ya kuundwa kwa serikali mpya ya umoja ambayo inatarajia kuamua juu ya utekelezaji wa mpango uliopendekezwa na Washington ifikapo Julai 1.

Wanadiplomasia wa Ulaya kwenye Baraza la Usalama walikumbusha Israeli juu ya uhalali wa mipaka iliyowekwa mnamo mwaka 1967 na kuionya Israeli kwamba itachukuliwa vikwazo kwa jaribio lolote la kuunganisha ardhi ya Ukinga wa Magharibi.
Wanadiplomasia wa Ulaya kwenye Baraza la Usalama walikumbusha Israeli juu ya uhalali wa mipaka iliyowekwa mnamo mwaka 1967 na kuionya Israeli kwamba itachukuliwa vikwazo kwa jaribio lolote la kuunganisha ardhi ya Ukinga wa Magharibi. AFP/Emmanuel Dunand
Matangazo ya kibiashara

Wanadiplomasia wa Ulaya kwenye Baraza la Usalama walikumbusha Israeli juu ya uhalali wa mipaka iliyowekwa mnamo mwaka 1967 na kuionya Israeli kwamba itachukuliwa vikwazo kwa jaribio lolote la kuunganisha ardhi ya Ukinga wa Magharibi.

Kutokana na marufuku ya kutotembea ambayo imewekwa katika hali ya kudhibiti janga hatari la Covid-19, mabalozi 5 kutoka nchi za Estonia, Ujerumani, Ubelgiji, Ufaransa na Poland wamekutana kwa mazungumzo kupitia video, na kuionya Israel kwa mpango wake huo.

"Tunashauri sana Israeli isichukue uamuzi peke yake ambao utapelekea kuunganisha ardhi yoyote ya Palestina inayokaliwa kimabavu. Uamuzi ambo utakuwa ni kinyume na sheria za kimataifa, " amesema Marc Pecsteen, balozi wa Ubelgiji kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Jaribio lolote la kuunganisha ardhi ya Palestina kwa Israeli, hata kwa msaada wa Marekani, litapelekea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulazimika kuchukuwa hatu kwa azimio, kulingana na na baadhi ya wanadiplomasia, ambao pia wanakumbusha kwamba suluhisho la serikali mbili lilitambuliwa na utawala mwingine wa chama cha Republican uliotangulia hapo zamani, utawala wa George Bush mnamo mwaka 2004.

Kwa upande mwingine kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesema Palestina haitazingatia tena makubaliano yoyote yaliotiwa saini na Israeli na Marekani kufuatia ahadi ya Israel ya kunyakua eneo Ukingo wa Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.