Pata taarifa kuu
MAREKANI-MASHARIKI YA KATI-AMANI

Trump azindua mpango wake wa amani kwa ajili ya Mashariki ya Kati

Rais wa Marekani Donald Trump amezindua mpango wake wa amani kwa ajili ya Mashariki ya Kati Jumanne wiki hii, mpango uliopongezwa kama wa "kihistoria" na Israeli lakini ambao umefutiliwa mbali na Palestina.

Pamoja na Benyamin Netanyahu, Jumatatu Januari 27 huko Washington, Donald Trump alisema anaamini kwamba mpango wake wa amani utafaanikiwa.
Pamoja na Benyamin Netanyahu, Jumatatu Januari 27 huko Washington, Donald Trump alisema anaamini kwamba mpango wake wa amani utafaanikiwa. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Trump amzindua mpango wake wa amani kwa ajili ya Mashariki ya Kati baada ya kukutana na Netanyahu na mpinzani wake kisiasa Benny Gantz mjini Washington.

Mpango huo unakuja wakati ambapo Trump anakabiliwa na kesi katika Baraza la Seneti, huku Netanyahu, ambaye anakabiliwa na mashitaka kuhusiana na tuhuma za ufisadi, akijiandaa kugombea katika uchaguzi wa mwezi ujao ambao Gantz anatarajia kushinda.

Mapema Jumatatu wiki hii Waziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh, ameyaomba mataifa yenye nguvu duniani kususia mpango wa amani wa Rais wa Marekani Donald Trump ambao wanauona kuwa unaipendelea sana Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.