Pata taarifa kuu
IRAN-UKRAINE-AJALI-HAKI

Iran kuwashughulikia waliohusika na udunguaji wa ndege ya abiria ya Ukraine

Mkanda wa video umeonesha namna makombora mawili ya Iran yalivyoangusha ndege ya abiria ya Ukraine wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu wote 176 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hassan Rouhani, na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Ali Khamenei, Tehran. (Picha kumbukumbu)
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hassan Rouhani, na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Ali Khamenei, Tehran. (Picha kumbukumbu) HO / KHAMENEI.IR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Iran imekiri kuwa ndege hiyo iliangushwa kwa bahati mbaya na uchunguzi unaendelea kuwachukulia hatua wale wote waliohusika.

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema watu wote wanaohusika na kuidungua bila ya kukusudia ndege ya Ukraine wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria na ajali hiyo itachunguzwa kwa umakini mkubwa.

"Kwa kuwa vikosi vyetu vimekiri makosa yao waziwazi na kuomba radhi kwa makosa yao. Ilikuwa hatua ya mwanzo na nzuri lakini hatua zinazofuata pia zitachukuliwa, " amesema rais wa Iran Hassan Rouhani.

Rais Rouhani pia ameagiza kuundwa kwa mahakama maalumu ya kushughulikia suala hilo itakayohusisha majaji na wataalamu wengi akisema kesi hiyo si ya kawaida na itakuwa ikifuatiliwa kote ulimwenguni.

Mahakama nchini humo imesema hii leo kwamba baadhi ya watu wanaohusika na ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 176 wamekwishakamatwa.

Taarifa iliyowekwa kwenye tovuti ya mahakama hata hivyo haikueleza ni watu wangapi wanashikiliwa ama majina yao.

Awali, Tehran ilikuwa imepinga kuhusika na tukio hilo ambalo lilitokea baada ya kuuawa kwa Jenerali wake wa kijeshi Kasem Soulemani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.