Pata taarifa kuu
SYRIA-UTURUKI-MAREKANi-USHIRIKIANO-USALAMA

Mashambulizi ya Uturuki Syria: Raia watoroka makazi yao

Mashambulizi ya jeshi la Uturuki dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi Kaskazini Mashariki mwa Syria yamesababisha maelfu ya raia kutoroka makazi yao.

Raia watoroka makazi yao kufuatia mashambulizi ya vikosi vya Uturuki dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi Kaskazini Mashariki mwa Syria.
Raia watoroka makazi yao kufuatia mashambulizi ya vikosi vya Uturuki dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi Kaskazini Mashariki mwa Syria. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Alhamisi wiki hii Marekani imebaini kwamba mashambulizi ya Uturuki mpaka sasa hayajafikia mstari mwekundu,.

Mapema wiki hii Rais wa Marekani Donald Trump aliruhusu Uturuki kuendesha operesheni ya kijeshi, huku akitangaza kuondoka kwa jeshi la Marekani waliokuwa wakipiga kambi kwenye mpaka kati ya Uturuki na Syria.

Donald Trump ameagiza Wizara ya Mashauriano ya Kigeni ya Mareakni kujaribu kushawishi Uturuki kusitisha mapigano dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi, kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa Marekani.

Mjini New York, baada ya mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, nchi tano za Ulaya, wanachama wa Baraza hilo - Paris, Berlin, Brussels, London, Warsaw - zimetaka Uturuki kusitisha mapigano hayo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea "wasiwasi wake mkubwa" kufuatia kuzuka kwa mapigano hayo.

Tangu Jumatano usiku, Ankara imezindua mashambulizi ya nchi kavu na vikosi vyake vimevuka mpaka, na kuimarisha operesheni yake katika maeneo ya mpaka ya Ras al-Ain na Tal Abyad, yanayodhibitiwa na waiganaji wa Kikurdi.

Wakati huo huo Rai wa Syria Bashar Al Asaad ameonya kuwa majeshi yake yako tayari kukabiliana na mashambulizi ya Uturuki kwa kulinda ardhi yake na uvamizi kutoka nje.

Vikosi vya Uturuki vimedhibiti vijiji kumi na moja karibu na miji hiyo miwili, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH).

Karibu wapiganaji 29 wa Kikurdi na raia 10 wameuawa katika mashambulizi ya roketi zilizorushwa kutoka miji ya mpakani, upande wa Uturuki, kama vile Akçakale, Makumi ya watu wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo, kwa mujibu wa OSDH.

Mashambulizi hayo yamesababisha watu zaidi ya 60,000, kutoroka makaazi yao kwenye maeneo ya mpakani tangu Jumatano wiki hii nchini Syria, OSDH imeogeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.