Pata taarifa kuu
ISRAELI-NETANYAHU-SIASA-USALAMA

Wananchi wa Israel wapiga kura, Netanyahu awania muhula wa tano

Wananchi wa Israeli wanapiga kura Jumanne hii Aprili 9, 2019 kuwachagua wabunge 120 wa Baraza la Wawakilishi (Knesset) na uchunguzi unaonyesha vyama vinavyomuunga mkono Waziri Mkuu anayemaliza muda wake Benjamin Netanyahu vinaibuka mshindi.

Wananchi wa Israeli wanapiga kura kuwachagua viongozi wao. Netanyahu anapambana na Benny Gantz.
Wananchi wa Israeli wanapiga kura kuwachagua viongozi wao. Netanyahu anapambana na Benny Gantz. REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Likud, chama cha mrengo wa kulia cha Benjamin Netanyahu, hata hivyo, kinapambana na chama cha mrengo wa kati "Blue and White" kinachoongozwa na Jenerali mstaafu ambaye ni maarufu nchini humo, Benny Gantz.

Tangu uchaguzi wa kwanza wa Israeli mnamo mwaka 1949, hakuna chama hata kimoja cha kisiasa kilichofanikiwa kupata wingi wa viti katika Baraza la Wawakilishi, hali ambayo wakati mwingine imekuwa ikisababisha mazungumzo ya muda mrefu kwa minajili ya uundwaji wa serikali ya umoja.

Kulingana na uchunguzi wa gazeti la kila siku la Yedioth Ahronoth uliyochapishwa Ijumaa wiki iliyopita, siku ya mwisho iliyoruhusiwa kuchapishwa kwa uchunguzi, chama cha Benny Gantz kinatarajia kupata viti 30 katika Baraza la Wawakilishi (Knesset), huku chama cha Likud kikipata 26.

Lakini vyama vya muungano wa mrengo wa kulia vinavyomuunga mkono Benjamin Netanyahu vinatarajia kupata viti 63 kati ya 120 katika Bunge hilo, idadi ndogo lakini inatosha kwa kupitisha sheria.

Ili kushiriki katika Bunge, chama kinapaswa kupata angalau 3.25% ya kura, ambayo ni sawa na viti vinne bungeni.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa saa 07:00 saa za Israeli (sawa na saa 04:00 saa za kimataifa) na zoezi la kupiga kura litamalizika saa 22:00 (sawa na 19:00 saa za kimataifa).

Baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi, rais Reuven Rivlin atawasiliana na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa na kuchagua yule anayeona ana uwezo wa kuunda serikali. Sio lazima kiongozi wa chama ambacho kimeshinda viti vingi.

Kiongozi atayechaguliwa atakuwa na siku 42 kutangaza serikali, vinginevyo rais ataomba mwingine kuchukuwa na fasi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.