Pata taarifa kuu
AFGHANISTANI-TALIBAN-MAUAJi-USALAMA

Watu kadhaa wauawa katika mashambulizi ya Taliban

Mamia ya wapiganaji wa Taliban wameendesha mashambulizi katika mkoa wa Badghis, magharibi mwa Afghanistan, na kusababisha vifo vingi upande wa vikosi vya usalama vya Afghanistan, maafisa wa serikali katika eneo hilo wamethibitisha leo Ijumaa.

Askari wa Afghanistan wakilinda mji wa Farah dhidi ya wapiganaji wa Taliban, Mei 2018.
Askari wa Afghanistan wakilinda mji wa Farah dhidi ya wapiganaji wa Taliban, Mei 2018. HAMEED KHAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi yameongezeka kwa miezi miwili iliyopita katika eneo hilo, ambalo, kwa mujibu wa viongozi wa mitaa, linaweza kuanguka mikononi mwa kundi la Taliban ikiwa hakuna msaada utakaotolewa kwa majeshi ya serikali.

Wapiganaji wa Taliban wameua askari 36 wa serikali na kuchukua udhibiti wa vituo kadhaa vya jeshi na polisi baada ya mashambulizi makubwa yaliyoanza Jumatano wiki hii, amesema Mkuu wa Wilaya ya Bala Murghab, Waris Sherzad.

Wapiganaji zaidi ya 30 wa Taliban pia wameuawa, msemaji wa gavana wa mkoa wa Badghis amesema.

Msemaji mmoja wa kundi hilo la Taliban, Yousuf Ahmadi, amedai kuwa Taliban ndio imetekeleza mashambulizi hayo, akisema kuwa yaliendeshwa kutoka maeneo mawili tofauti na yameruhusu udhibiti wa vituo vitano vya usalama.

Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan imesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba vikosi vya Afghanistan vimeondoka kwenye vituo vya usalama kwa uamuzi wa kimkakati ili kuepuka maafa zaidi kwa upande wa raia.

Wizara hiyo imeongeza kuwa imeomba kufanyike mashambulizi kadhaa ya angani dhidi ya ngome za Taliban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.