Pata taarifa kuu
YEMEN-UN-USALAMA-MAZUNGUMZO

Mazungumzo kuhusu Yemen kuanza Jumatano Sweden

Wajumbe wa waasi wa Houthi wanatarajiwa hivi karibuni huko Sweden, ambapo mazungumzo yanatarajiwa kuanza, labda Jumatano, ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoikumba Yemen.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, mwanadiplomasia kutoka Uingereza Martin Griffiths, aliwasili Sanaa Jumatatu wiki hii ili kuongozana na ujumbe wa waasi kwenda Sweden.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, mwanadiplomasia kutoka Uingereza Martin Griffiths, aliwasili Sanaa Jumatatu wiki hii ili kuongozana na ujumbe wa waasi kwenda Sweden. REUTERS/Abduljabbar Zeyad
Matangazo ya kibiashara

Afisa mmoja wa Houthi ameliambia shirika la Habari la Reuters kwamba ujumbe wa waasi ulikuwa unatarajiwa kuondoka Sanaa Jumatatu usiku au Jumanne asubuhi.

Waasi wa Kishia wanaoungwa mkono na Iran, ambao wamekuwa wanadai kuwa baadhi ya wapiganaji wao waliojeruhiwa wasafirishwe kwenda nchini Oman ili waweze kushiriki mazungumzo, madai yao yamepatiwa jibu.

Mpiga picha wa Reuters anasema ameona kundi la wapiganaji 50 waliojeruhiwa wakiwasili mapema Jumatatu asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Sanaa kwa ndege iliyoyokodiwa na Umoja wa Mataifa. Ndege hiyo iliendelea na safari yake hadi nchini Oman.

Umoja wa nchi za Kiarabu umesema umekubali kuondolewa kwa wapiganaji hao kwa sababu za kibinadamu na kujenga imani kati ya pande znazokinzana kabla ya mazungumzo.

Mwezi Machi 2015 Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu waliongoza muungano wa kijeshi kusaidia serikali ya Rais wa Yemen Abd-Rabbo Mansour Hadi dhidi ya ya waaasi wa Houthis ambao wanahibiti Sanaa, mji mkuu wa nchi hiyo.

Tangu wakati huo, vita vimesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha. Watu 10,000 waliuawa katika vita hivyo kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwishoni mwa mwaka 2016 na vita hivyo vimewaacha raia katika janga kubwa la njaa.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, mwanadiplomasia kutoka Uingereza Martin Griffiths, aliwasili Sanaa Jumatatu wiki hii ili kuongozana na ujumbe wa waasi kwenda Sweden.

Kwa wiki kadhaa, anataka kufufua mchakato wa amani baada ya kushindwa kwa jaribio la kwanza mapema mwezi Septemba mjini Geneva, ambapo waasi wa Houthi hawakutu awawkilishi wao.

Wawakilishi wa serikali ya Yemen watawasili nchini Sweden baada ya ujumbe wa waasi kuwasili.

Mazungumzo yanaweza kuanza Jumatano wiki hii, kwa mujibu wa vyanzo rasmi.

Nchi za Magharibi, ambazo zinaoa silaha na taarifa mbalimbali kwa muungano wa nchi za Kiarabu, zinaunga mkono jitihada za amani, licha mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia na mkosoaji mkubwa wa utawala wa kifalme nchini humo, Jamal Khashoggi, Oktoba 2 katika ubalozi mdogo mjini Istanbul yaliyosababisha hasira dhidi ya Riyadh.

Bunge la Seneti la Marekani linataraji wiki hii kujadili azimio linaloitaka Marekani kusitisha uungwaji wake mkono kijeshi kwa muungano wa nchi za Kirabu unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen.

Wakati huo huo Iranimesema inaunga mkono mazungumzo ya amani nchini Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.