Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Mfalme Salman aunga mkono juhudi za amani Yemen

Mfalme wa Saudi Arabia, Salman katika taarifa yake ya kwanza kwa umma tangu kuanza kwa kesi ya Khashoggi, amesema Jumatatu wiki hii kwamba anaunga mkono jitihada za Umoja wa Mataifa za kumaliza vita nchini Yemen.

Mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz Al Saud.
Mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz Al Saud. AFP/Oscar Del Pozo
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na Baraza la Shura, mkutano wa wajumbe150 wanaohusika na kumshauri kiongozi wa nchi hiyo, Mfalme Salman, mwenye umri wa miaka 82 amomba kwa mara nyingine jumuiya ya kimataifa kuishinikiza Iran kusitisha mara moja mipango yake ya kutengeneza silaha za nyuklia na majaribio ya makombora ya masafa marefu.

Wakati wa hotuba yake hakutaja moja kwa moja mgogoro uliosababishwa na mauaji ya mwandishi wa habari kutoka Saudi na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Mfalme Slaman, Jamal Khashoggi, aliyeuawa kikatili katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, nchini Uturuki tarehe 2 Oktoba mwaka huu.

Hata hivyo, amesifu mfumo wa mahakama za Saudi Arabia. "Tunajivunia juhudi zote zinazotumiwa na majaji na waendesha mashitaka kwa kutimiza wajibu wao," amesema.

Shirika la ujasusi la Marekani la CIA linaamini kwamba mwanawe, Mwanamfalme Mohamed bin Salman, aliamuru Jamal Khashoggi auawe. Kwa upande mwingine, ofisi ya mwendesha mashitaka ya Saudi Arabia imehakikisha kwamba ilikuwa "hajui chochote".

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen, Martin Griffiths, anajaribu kufufua mchakato wa amani baada ya kushindwa mwezi Septemba huko Geneva, ambapo waasi wa Houthi hawakushiriki mazungumzo hayo. Anatarajia kuwakusanya wadau katika mgogoro wa Yemeni katika mkutano wa amani mwishoni mwa mwaka huu nchini Sweden.

Sikua ya Jumapili waasi wa Houthi nchini Yemen walitangaza rasmi kwamba wako tayari kusitisha mashambulizi ya aina yoyote dhidi ya Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kirabu (UAE).

Waasi hawa wa Kishia wanaoungwa mkono na Iran wamesema wako tayari kukubali kusitisha mapigano kama muungano wa nchi zenye madhehebu ya Kisuni, unaoongozwa na Saudi Arabia "unataka kweli amani".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.