Pata taarifa kuu
UJERUMANI-SAUDI ARABIA-VIKWAZO

Mauaji ya Khashoggi: Maafisa 18 wa Saudia wawekewa marufuku ya kuingia Ujerumani

Ujerumani imeamuru kuwawekea marufuku maafisa 18 wa Saudi Arabia kuingia nchini humo. Ujerumani inawashtumu maafisa hao kuhusika katika mauaji ya mwandishi na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Mfalme wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi katika ubalozi mdogo wa nchi hiyo katika mji wa Istanbul, nchini Uturuki.

Saudi Arabia inaendelea kukabiliwa na vikwazo kufuatia mauaji ya mwandishi na mkosoaji wa utawala wa Mfalme Salman, Jamal Khashoggi, aliyeuawa katika ubalozi mdogo wa Saudia Uturuki.
Saudi Arabia inaendelea kukabiliwa na vikwazo kufuatia mauaji ya mwandishi na mkosoaji wa utawala wa Mfalme Salman, Jamal Khashoggi, aliyeuawa katika ubalozi mdogo wa Saudia Uturuki. REUTERS/Simon Dawson
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa mamlaka ya Ujerumani ni pamoja na vikwazo vya silaha vilivyowekwa na Berlin kuhusu mauzo ya silaha kwa Saudi Arabia kwa kusubiri ufafanuzi zaidi wa mazingira ya mauaji hayo.

Msimamo wa Ujerumani hauhusu nchi 25 wanachama wengine wa eneo la Schengen ambao wanaendelea kudhibiti mipaka yao.

Hata hivyo, Ujerumani inatarajia kuhimiza Umoja wa Ulaya kuchukuwa vikwazo zaidi dhidi ya utawala wa Saudi Arabia.

"Sisi tunashirkiana kwa karibu na marafiki zetu Ufaransa na Uingereza na tuliamua kuweka katika mfumo wa Schengen alama ya marufu mbele ya majina yao," amesema Christofer Burger, msemaji wa Wizara yaMambo ya Nje ya Ujerumani.

Ufaransa ni sehemu ya eneo la Schengen lakini Uingereza haimo.

Maafisa 15 wa timu ambayo ilikwenda Istanbul kwa mauaji ya Jamal Khashoggi wako kwenye orodha hiyo pamoja na watu wengine watatu wanaoshukiwa kuwa walipanga mauaji hayo. Majaina yao hayakuwekwa wazi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ameongeza kuwa marufuku itatumika kwa wamiliki wa pasipoti za kidiplomasia wanazotumia wengi kati ya familia ya kifalme nchini Saudi Arabia.

Christofer Burger alikataa kusema chochote kuhusu ripoti katika vyombo vya habari vya Marekani kwamba shirika la ujasusi la Marekani (CIA) liliweza kuhitimisha kuwa mauaji ya Khashoggi yalifadhiliwa moja kwa moja na Mwanamfalme Mohammed bin Salman.

Mahakama ya Saudi Arabia ilisema wiki iliyopita kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman, ambaye ndiye mtawala wa ufalme, hakuhusika katika mauaji ya Khashoggi.

Msemaji wa Wizara ya Uchumi ya Ujerumani amesema kuwa vikwazo vya sialaha dhidi ya utawala wa kifame wa Saudi Arabia vitaendelea kutumika. "Hakuna mauzo ya silaha kutoka ya silaha kutoka Ujerumani kwenda Saudi Arabia kwa sasa," amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.