Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-UTURUKI-MAZUNGUMZO

Putin na Erdogan waridhishwa na mkutano wa Sochi kuhusu Syria

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wamesema leo Jumatano kuwa"wameridhishwa" na mkutano kuhusu Syria uliofanyika siku moja kabla, Ikulu ya Kremlin imetangaza licha ya kutokua na matokeo halisi.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura, atoa tangazo baada ya mazungumzo ya kitaifa baina ya Wasyria, Januari 30, 2018 Sochi, Urusi.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura, atoa tangazo baada ya mazungumzo ya kitaifa baina ya Wasyria, Januari 30, 2018 Sochi, Urusi. AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wawili, ambao walizungumza kwenye simu, "walionyesha kuridhika kwa matokeo ya mazungumzo ya kitaifa baina ya wadu wote nchini", yaliyofanyika siku ya Jumanne katika mji wa Sochi nchini Urusikwa jitihada za Moscow, Ankara na Tehran, taarifa hiyo imesema.

"Wamesisitiza umuhimu wa kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa" katika mkutano huu kati ya wawakilishi wa mashirika ya kiraia na vyama vya kisiasa kutoka Syria, ambao "wanalenga kuendeleza mchakato wa utatuzi wa kisiasa nchini Syria", kulingana na chanzo hicho.

Mkutano wa Sochi ambao ulisusiwa na makundi makuu ya upinzani kutoka Syria, Wakurdi na nchi za Magharibi, ulikutanisha pamoja wawakilishi wa chama cha tawala cha Ba'ath kilichowakilisha serikali, washirika wake na upinzani wenye msimamo wa wastani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.