Pata taarifa kuu
MAREKANI-ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Marekani kuanzisha upya mchakato wa amani Mashariki ya Kati

Hitimisho la "makubaliano ya mwisho" kati ya Waisraeli na Wapalestina ilikuwa nia iliyoelezwa na Donald Trump miezi michache iliyopita. Ujumbe wa Marekani katika ngazi ya juu uliwasili Jumatano jioni Mashariki ya Kati.

Ujumbe wa Marekani unatarajia kukutana na Mahmoud Abbas siku ya Alhamisi, Agosti 24.
Ujumbe wa Marekani unatarajia kukutana na Mahmoud Abbas siku ya Alhamisi, Agosti 24. ABBAS MOMANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jason Greenblatt, Jared Kushner na Dina Powell,washirika watatu wa karibu wa rais wa Marekani, watakutana na viongozi wa Israel katika mji wa Jerusalem na Mahmoud Abbas rais wa Mamlaka ya Palestina katika mji wa Ramallah Alhamisi hii 24 Agosti.

Rais wa Marekani Donald Trump aliahidi kuanzisha mchakato wa amani kwa nchi hizi mbili. Ni matarajio makubwa ya viongozi wa Palestina. Donald Trump alionekana kujitenga kwa kile ambacho ni kanuni ya muongozo wa jumuiya ya kimataifa.

Israel inaendelea kushikilia baadhi ya maeneo ya Palestina kinyume na sheria huku sheria ya kimataifa ikivunjwa, hata utawala mpya wa Marekani haujakemea hilo.

Msimamo wa Marekani unalegalega

Wapalestina hawana matumaini yoyote na jitihada hizo za Marekani: "nlikutana mara kadhaa na wajumbe wa Donald Trump lakini bado sijaelewa msimamo wao," alisema hivi karibuni Mahmoud Abbas.

Rais wa Mamlaka ya Palestina atahitaji majibu ya maandishi kutoka kwa ujumbe wa Marekani juu ya maswala haya. Maswali yanayotakiwa kuwa masharti ya kurudi kwenye meza ya mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.