Pata taarifa kuu
ISRAEL-MAREKANI-PALESTINA-USHIRIKIANO

Rais Trump amtuma mjumbe wake Mashariki ya Kati

Mwakilishi maalum wa Rais Trump kwa mazungumzo ya kimataifa Jason Greenblatt alisafiri kwenda Israel jana usiku katika hali ya kuunga mkono juhudi za kupunguza mvutano katika ukanda wa Mashariki ya Kati," afisa mmoja wa Marekani amesema.

Donald Trump, rais wa Marekani.
Donald Trump, rais wa Marekani. REUTERS/Kacper Pempel
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati ambapo kuliskika risasi kwenye ubalozi wa Israel nchini Jordan na raia wawili wa Jordan na raia mmoja wa Israel amejeruhiwa katika ufyatuliaji huo risasi.

Polisi iimezingira ubalozi wa Israel katika mji wa Amman na Israel imechukua uamuzi wa kumewahamisha wafanyakazi. Ubalozi huo wenye ulinzi mkali uko mtaa wa Rabiyeh ambalo ambao ni wa kifahari mjini Amman

Ufyatuaji huo ulitokea katika jengo moja linalotumiwa na ubalozi wa Israel.

Inaarifiwa kuwa watu hao walikuwa wakifanya kazi na kampuni moja ya zamani na waliingia ndani ya ubalozi wa Israel kabla ya ufyatuaji risasi kuanza, kwa mujibu wa polisi.

Israel haijazungumzia kisa hicho. Ripoti chache zimetolewa kuhusu kile kilisababisha kutokea kwa kisa hicho.

Itakumbukwa kwamba siku ya Ijumaa umati wa watu uliingia mitaani mjini Amman kupinga hatua ya Israeal ya kuweka vifaa vya kutambua chuma katika aneo takatifu kwa waislamu na wakiristo mashariki mwa Jerusalem.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.