Marekani yasema Syria inapanga kutumia silaha za kemikali kuwashambulia raia
Marekani inasema serikali ya Syria inafanya maandalizi ya kuwashambulia raia wa kawaida kwa kutumia silaha zake za kemikali.
Imechapishwa:
Ikulu ya Marekani imesema uchunguzi wake umeonesha wazi kuwa maandalizi yanafanyika kutekeleza shambulizi hilo kama ilivyokuwa mwezi Aprili mwaka huu na kusababisha maafa makubwa ya watu.
Wsshington DC sasa inaonya kuwa itaichukulia hatua kali serikali ya rais Bashar Al Assad ikiwa itatekeleza shambulizi hilo.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley amesema Urusi na Iran pia watawajibikia shambulizi hilo litatokea.
“Shambulizi lolote kwa raia wa Syria, tutailaumu serikali ya Urusi na Iran ambayo inamuunga mkono rais Bashar Al Assa", amesema Nikki.
Serikali ya Damascus hata hivyo imekuwa ikikanusba madai yoyote ya kutumia silaha zake za nyuklia kuwashambulia raia wa nchi hiyo.