Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI-USALAMA

Raia 20 wauawa katika mashambulizi ya muungano Syria

Mashambulizi ya anga yanayoendeshwa na muungano wa kimataifa dhidi ya makundi ya kijihadi katika mkoa wa Syria wa Deir Ezzor yamewaua raia 20, shirika la Haki za Binadamu nchini Syria la OSDH limearifu.

Maelfu ya raia ambao bado wanaishi katika sehemu ya jimbo la Deir Ezzor na vijiji jirani vilio chini ya udhibiti wa vikosi vya serikali.
Maelfu ya raia ambao bado wanaishi katika sehemu ya jimbo la Deir Ezzor na vijiji jirani vilio chini ya udhibiti wa vikosi vya serikali. REUTERS/Khalil Ashawi
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi yaliyoendeshwa siku ya Jumatatu usiku kwenye mji wa Abu Kamal, karibu na mpaka wa Iraq, kwa mujibu wa OSDH, ambayo inasema kwamba wapiganaji watatu wa kundi la Islamic State (IS), ambalo linadhibiti wilaya hiyo, pia walipoteza maisha.

Mapema mchana, mashambulizi mengine yaliwaua raia saba, ikiwa ni pamoja na watoto, katika kijiji cha Husseiniyé, imeongeza OSDH.

Muungano unaoongozwa na Marekani unaendesha mashambulizi ya angani dhidi ya kundi la IS nchini Syria tangu mwaka 2014 na umekua ukisaidia jamii ya Kiarabu ya Wakurdi kwa kuendelea na vita kuelekea ngome ya wanamgambo hao ya Raqa.

Mwezi Machi, watu wasiopungu 220 waliuawa "katika mashambulii yalioendeshwa kimakosa dhidi ya IS nchini Iraq na Syria tangu 2014. Lakini mashirika ya kimataifa wanaamini kwamba idadi halisi ni kubwa zaidi.

Sehemu kubwa ya mkoa wa Deir Ezzor, ulio tajiri kwa mafuta, unadhibitiwa na kundi la kiislamu la madhehebu ya KIsunni, ikiwa ni pamoja na sehemu ya mji mkuu wa mkoa huo.

Wanajihadi wanazingira maeneo ya serikali ya mji wa Deir Ezzor,.

Vita nchini Syria vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 320,000 na mamilioni kulazimika kuyahama makazi yao tangu kuzuka kwa vita hivyo mwezi Machi 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.