Pata taarifa kuu
QATAR-DIPLOMASIA-USALAMA

Qatar yatengwa na Mataifa sita ya Kiarabu

Mataifa sita ya Kiarabu yakiongozwa na Saudi Arabia na Misri, yamesitisha ushirikiano wa kidiplomasia na nchi ya Qatar kwa madai kuwa inaunga mkono makundi ya kigaidi.

Qatar
Qatar REUTERS/Fadi Al-Assaad/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Qatar imeshtumiwa kuunga mkono makundi kama Islamic State na al-Qaeda, ambayo yanaendelea kuwa tishio kwa usalama wa eneo la Mashariki ya Kati.

Mataifa mengine yaliyotangaza hatua hiyo ni pamoja na Bahrain, Falme za Kiarabu, Yemen na Libya.

Qatar imekanusha madai hayo na kusema, hakuna ushahidi wowote kuonesha kuwa inashirikiana na makundi hayo na inahatarisha usalama Mashariki ya Kati.

Mataifa hayo ya kiarabu yamesema yamechukua hatua hiyo kwa maslahi yao ya kitaifa pamoja na maswala ya kiusalama.

Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Bahrain zimewataka raia wa Qatar kuondoka nchini humo ndani ya wiki mbili.

Uturuki imesema iko tayari kuongoza mazungumzo kati ya Qatar na Mataifa hayo ya kiarabu.

Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema kilichotokea kati ya nchi hizo za kiarabu na Qatar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.