Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAEL-HAKI

Zaidi ya Wapalestina 1,000 wanaozuiliwa Israel waanza mgomo wa kula

Zaidi ya wafungwa 1,000 wa Palestina wanaozuiliwa katika magereza ya Israel wameanza mgomo wa pamoja wa kukataa kula Jumatatu hii, wakifuata wito wa Marwan Barghouthi, kiongozi wa harakati za kidini aliyehukumiwa kifungo cha maisha jela, amesema afisa wa Palestina.

Raia huyu wa Palestina akishiilia mkonononi picha ya Marwan Barghouthi, kiongozi wa harakati za kidini aliyehukumiwa kifungo cha maisha jelawakati wa maadhimisho ya"Siku ya wafungwa," Aprili 16, 2015 katika Gaza.
Raia huyu wa Palestina akishiilia mkonononi picha ya Marwan Barghouthi, kiongozi wa harakati za kidini aliyehukumiwa kifungo cha maisha jelawakati wa maadhimisho ya"Siku ya wafungwa," Aprili 16, 2015 katika Gaza. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Takribani wafungwa 1,300 wa Palestina wameanza mgomo wa kususia chakula na idadi hii inaweza kuongezeka katika masaa yajayo," Qaraqee Issa, anayehusika na swala la wafungwa katika Mamlaka ya Palesina, ameliambia shirika la habari la AFP.

"Kwa mujibu wa habari ambazo tunazo kwa sasa, wafungwa 1,500 wamekataa kula" kwa kukemea mazingira ambamo wanazuiliwa, Sarahneh Amani, msemaji wa shirika linalotetea wafungwa wa Palestina, ameliambia kwa upande wake shirika la habari la AFP.

Msemaji wa mamlaka ya magereza ya Israel, Assaf Librati ameiambia AFP kuwa "wafungwa 700 walitangaza jana (Jumapili) nia yao ya kuanza mgomo wa kususia chakula."

Jumatatu asubuhi mamlaka wa magereza umeendesha uchunguzi ili kjua ni wafungwa wa ngapi wanaokataa kula, kwani kuna baadhi ambao wanaweza kuwa wametangaza hivyo na kisha kurudi kuanza kula."

Bw Librari hakutoa maelezo zaidi, lakini kwa mujibu washirika linalotetea wafungwa, "Mamlaka ya wa magereza imewapokonya wafungwa hao bidhaa zao zote zilizokuwa katika sehemu wanakozuiliwa na imeanza kuhamisha wafungwa kwenye magereza mengine ".

Mgomo usiojulikana muda utakao malizika umeanzishwa wakati ambapo ikiadhimishwa "Siku ya wafungwa," inayosheherekewa kila mwaka na Wapalestina kwa zaidi ya 40 miaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.