Pata taarifa kuu
SYRIA-TRUMP-USALAMA-SIASA

Upinzani wa Syria: Tuna imani kuwa Trump atamaliza mgogoro wa kisiasa Syria

Upinzani nchini Syria unasema kuwa, unaamini kuwa rais mpya wa Marekani Donald Trump atasaidia pakubwa kumaliza mzozo katika nchi yao.

Askari wa Syria wakitazama vifuzi vya Hekalu ya Bel, katika mji wa kale wa Palmyra, April 1, 2016.
Askari wa Syria wakitazama vifuzi vya Hekalu ya Bel, katika mji wa kale wa Palmyra, April 1, 2016. REUTERS/Omar Sanadiki
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa wa muungano huo wanaoishi nje ya nchi yao wakizungumza jijini Geneva wakiongozwa na kiongozi wa ujumbe wao Nasr al-Hariri awmesema kuwa kwa sasa kila mmoja anasubiri kauli ya Trump.

Mazungumzo ya amani yamekuwa yakiendelea tangu wiki iliyopita lakini wajumbe wa serikali na upinzani hawajaanza mazungumzo ya ana kwa ana huku Urusi ambayo ni mshirika wa karibu wa rais Bashar Al Assad ikishtumu upinzani kwa kutoonesha moyo wa kufanikisha mazungumzo hayo.

Hayo yanajiri wakati Rais Bashar Al Assad amemteua Makamu wake Bakri Hassan Saleh kuwa Waziri Mkuu.

Bwana Saleh ni mmoja wa mshirika wa karibu zaidi wa Bashir, na alihusika katika mapinduzi ya mwaka 1989 yaliyomleta mamlakani Omar Al Bashir.

Rais Bashir Al Assad amebuni cheo cha waziri mkuu, ambacho aliifutilia mbali mara tu baada ya kuingia madarakani kupitia mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.